Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Sunday, October 24, 2021

NETFLIX WATOA TAKWIMU.

 


#UNAAMBIWA Kwa mujibu wa Netflix Mtu mmoja pekee kati ya Watu 100 anaweza kufanikiwa kumaliza kutazama movie ya Veronica mwanzo mwisho, ni movie ambayo iliingizwa sokoni mwaka 2017 na inatajwa kuwa ndio movie yenye matukio ya kutisha na yanayoogopesha kuliko movie zote.


Veronica ni Filamu ya Kihispania ambayo imefanywa na Director Paco Plaza ikihusu maisha ya kweli ya Mtoto wa kike Estefania Lazaro ambaye alifariki mwaka 1992.

Mliotazama hii movie mtuambie, ni BIG YES au BIG NO?


Friday, October 22, 2021

BIG SEAN APIGA PICHA NA NYUKI 65,000 MWILINI.


 inapokuja suala la kufanya chochote ili upate kitu kizuri chenye uhalisia basi hilo sio gumu kabisa kwa mastaa hasa wasanii wa muziki kwenye kazi zao.


Moja ya picha zinazotrend mtandaoni kwasasa ni hii kutoka kwa @bigsean, ambaye ni rapa kutoka Marekani. Mkali huyo ame-share picha yake akiwa na kundi la nyuki wakati ana shoot video ya wimbo wake mpya uitwao “What A Life” ambao anatarajia kuuachia.

Kwenye maelezo yake @bigsean ameeleza kuwa picha hiyo ni yakweli na sio yakutengeneza, pia amedai idadi ya nyuki hao walikuwa ni Elfu 65,000.

ALEC BALDWIN AMEUUA MWANAMKE WAKATI WA KUTENGEZA FILAMU.


 Nyota wa sinema za Hollywood Alec Baldwin ameua mwanamke mmoja na kumjeruhi mwanaume kimakosa alipofyatua bunduki ya maigizo wakati wa kutengezwa filamu huko New Mexico.


•
Mwanamke huyo ametajwa kama Halyna Hutchins, 42, ambaye alikuwa akifanya kazi kama mkurugenzi wa upigaji picha.

•
Mtu anayetibiwa ni Joel Souza, 48, mkurugenzi wa filamu.

•
Polisi katika jimbo hilo la Marekani walisema Bw. Baldwin alitoa silaha hiyo wakati wa utengezaji wa filamu yake.

•
Msemaji wa Bw Baldwin aliliambia shirika la habari la AP kwamba kisa hicho kilihusisha utumiaji mbaya wa bunduki ya maigizo.

•
Polisi bado wanachunguza tukio hilo huko Bonanza Creek Ranch, eneo maarufu la utengenezaji wa sinema, na hakuna mashtaka yoyote yaliyofunguliwa dhidi yake.

DIAMOND KUWANIA TUZO ZA MTV EUROPE MUSIC AWARDS.


 Nyota muziki wa Bongoflava na Tanzania, Diamond Platnumz @diamondplatnumz amechaguliwa kuwania tuzo za MTV Europe Music Awards (MTV EMA) 2021.


•
‘Simba’ atachuana na wasanii wengine wanne kutoka Afrika, Tems (Nigeria), Wizkid (Nigeria), Focalistic (Afrika Kusini) na Amaarae (Ghana) kuwania taji la mwaka huu la Best African Act.

•
Katika hatua itakayowaacha wapenzi wa muziki wa kiafrika vinywa wazi, Nyota mwingine wa Afrika ambaye pia ni mshindi wa Grammy, Burna Boy hakutajwa katika kitengo chochote.

•
Washindi watatuzwa katika hafla itakayoandaliwa Papp László Budapest Sportaréna jijini Budapest, Hungary, November 14 .

AISHI MANULA AMESHINDA TUZO YA GOLIKIPA BORA WA MSIMU WA 2020/2021.


 Kipa wa Simba SC Aishi Salum Manula ameshinda tena Tuzo ya Golikipa bora wa msimu wa 2020/2021 katika Tuzo za TFF zinazotolewa usiku huu Dar es salaam

FEISAL TOTO ASHINDA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MASHINDANO YA KOMBE LA SHIRIKISHO.


 Tuzo za TFF bado zinaendelea kutolewa usiku huu Dar es salaam ambapo Mshindi mwingine aliyetajwa ni Mchezaji wa Yanga Feisal Salum @Feisal194 ambae ameshinda Tuzo ya Mchezaji bora wa mashindano ya Kombe la Shirikisho.

BOCCO ANG`ARA TENA KWENYE TUZO ZA TFF 2020/2021


 Waziri Mkuu wa Tanzania @kassim_m_majaliwa akimkabidhi Mshambuliaji wa Simba SC John Bocco tuzo ya (MVP) Mchezaji bora wa mashindano ya Ligi Kuu soka Tanzania bara 2020/2021

 
 
Blogger Templates