Benjamin Solomon Carso alizaliwa katika eneo la Detroit katika jimbo
la Michigan.
Mama yake, Sonya Carson, aliacha shule akiwa katika daraja la tatu na kuolewa
na Robert Solomon Carson, aliyekuwa mchungaji mzee zaidi katika eneo la
Tennesee, wakati mama yake Ben akiwa na umri wa miaka kumi na tatu tu (13).
Wakati Carson akiwa na umri wa miaka nane tu (8), wazazi wake waliachana. Mama
Carson aliachiwa kuwalea Benjamin na kaka yake Curtis, yeye mwenyewe. Alifanya
kazi katika sehemu mbili au hata tatu kwa mara moja ili aweze kuwatosheleza
watoto wake wawili. . Mwanzoni Carson alikuwa na maisha magumu shuleni.
, hali iliyopelekea kuwa wa mwisho mara kadhaa katika darasa lake. Alikuwa
akiitwa majina mbalimbali kutokana na hali hiyo, hivyo ikapelekea kukua kwa
hasira kali ndani yake. Akiwa amedhamiria kubadilisha maisha ya familia yao,
mama yake akamzuia Carson muda wake wa kuangalia runinga na kumzuia kutoka nje
kila siku hadi pale atakapokuwa amemaliza kazi zake za shule kila siku. Mama
yake alimtaka Carson Kusoma vitabu viwili kutoka maktaba na kuandika taarifa
juu ya vitabu hivyo kila wiki, bila kujali elimu yake ndogo, hata hivyo
hakuweza kusoma vitu ambavyo vilikuwa vmeandikwa.
Lakini mapema, Carson alimshangaza mwalimu wake na wanafunzi
wenzake kutokana na maendeleo yake. Anakumbuka “Ni wakati ule ndipo
nilipogundua kuwa sikuwa mpumbavu” anagundua baadae. Carson anaendelea
kuwashangaza wanafunzi wenzake na ndani ya mwaka mmoja alikuwa na ujuzi na kuwa
katika nafasi ya juu katika darasa lake.
Baada ya kugundua kuwa alitaka kuwa daktari wa magonjwa ya
akili kwa lengo la kutoa msaada kwa watu wenye magonjwa ya akili ndani yam ji
anaoishi, Carson alimaliza shule na matokeo mazuri yenye heshima na hivyo
alijunga na chuo kikuu cha Yale ambapo alipata shahada yake ya kwanza katika maswala
ya saikolojia ya akili. Pschology. Baada ya kutoka Yale,
aliendelea na shule ya udaktari ya michigan, ambapo hapo ndipo nia yake ya kuwa
daktari wa magonjwa ya akili ilipobadilika na kuwa daktari wa mishipa. Uwezo
wake mkubwa wa kuona na uwezo wake wa kufikiri haraka ulimfanya awe daktari wa
upasuaji mzuri zaidi Baada ya kumaliza shule yake ya udaktari, alikuwa daktari
wa mishipa msaidizi katika hospitali ya Johns Hopkins katika jimbo la
Baltimore. Akiwa na umri wa miaka 33, alikuwa profesa wa hospitali na pia
mkurugenzi wa idara ya upasuaji mishipa ya Watoto.
Mwezi wa tisa mwaka 1987, Carson alifanya upasuaji wa
kutenganisha mapacha wenye umri wa miezi saba, waliokuwa wameungana katika
sehemu ya kichwa. Carson alikuwa ndiye kiongozi wa upasuaji huo mgumu, Mwaka
1997, Carson pamoja na timu yake, walienda Afrika ya Kusini, kuwatenganisha
Lukas na Joseph Banda kutoka Zambia. Watoto wote wawili waliweza kuishi baada
ya upasuaji na hakuna hata mmoja wao aliyepata uharibifu wa ubongo. Watoto hao
wa Banda walikuwa ni watoto wa kwanza walioungana kwa upande wa juu wa vichwa
vyao kuweza kuishi baada ya upasuaji. Upasuaji huo ulifanyika kwa saa 28. Mwaka
2003, Carson alikuwa moja kati ya madaktari waliofanya upasuaji wa watu wazima
waliokuwa wameungana katika sehemu ya vichwa, Ladan na Laleh Bijan.
Lakini wote hawakuweza kuishi baada ya upasuaji. Alipoulizwa kwa nini alikubali
kufanya upasuaji wa kubahatisha kiasi hicho alisema, ndugu hao walikuwa
wamekubali bora wafe kuliko kuendelea kuishi wakiwa wameungana.
Carson amepokea tuzo mbalimbali katika miaka mbalimbali,
kama vile, Shahada za heshima za Udaktari 40, pia ni mwanachama katika chama Chuo
Kikuu cha Mafanikio ya Marekani, Chama cha Wamarekani Wanajulikana wa Horatio,
Alpha Omega Alpha Waheshimu Medical Society Ushirikiano wa yele, (Bodi ya
wakurugenzi wa Chuo kikuu cha Yale) na mashirika mengine mengi. Pia ni
mwanzilishi na mkurugenzi wa Mfuko wa Somo la Carson , ambao huwasaidia
wanafunzi kutoka katika historia tofauti tofauti walio na vipaji maalumu katika
masomo. Mwaka 2007, Carson alijumuishwa katika Chuo kikuu cha Indiana Wesley
Society ya Dunia Mabadiliko na kupokea nishani ya heshima wa udaktari wakati
akizungumza katika Chuo. Aliporudi, alirudi na rafiki yake Tony Dungy ambaye
naye alikumuishwa katika jamii. Tarehe 19 mwezi wa 9 mwaka 2008, Carson
alopokea nishani ya raisi ya uhuru kutoka kwa Raisi George
W. Bush
Carson ameandika vitabu vitatu vilivoongoza katika mauzo na
vilivyochapishwa na Zondervan shirika la kimataifa
la uchapaji la kikristo, Vinavoitwa : Gifted Hands (Mikono Yenye Vipawa: Hadithi
Ya Ben Carson) , The Big Picture, na Think Big Kitabu cha kwanza cha
Historia ya maisha ya mtu, na vitabu vingine viwili ni kuhusu filosofia ya
maisha yake hususani katika mafanikio yake yanayoenda sambamba na imani yake
kwa Mungu.Carson ni Mkristu katika dhehebu la sabato.
Mwaka 2002, Carson aliamuriwa kusitisha kuonekana katika
maeneo yenye umati wa watu, baada ya kupata matatizo ya kiafya ya kwake
mwenyewe. Mwezi wa sita alikutwa na dalili za kuwa na Saratani ya Kibofu cha
mkojo, lakini kwa bahati nzuri, saratani hiyo iliweza kukutwa katika muda
muafaka. Lakini pamoja na hayo, Carson alibadilisha mfumo wake wa maisha, Bado
anafanya upasuaji kwa zaidi ya watoto mia tatu (300) kwa mwaka lakini amekuwa
akijaribu kupunguza muda wake.Carson amekuwa akifanya kazi kuanzia saa 7:00
asubuhi na kumaliza saa 8:00 usiku, lakini tangu agundulike kuwa na saratani
amekuwa akifanya kazi na kuondoka saa 6:15, jioni. Hii inampa muda zaidi wa
kukaa na mke na watoto wake watatu (3)
Makala ya video kuhusu maisha ya Carson inyoitwa Gifted
Hands:Kitabu kinachohusu, hadithi ya Ben Carson kilitolewa na Zondervan mwaka
1992, hali iliyopelekea mwaka 2009, filamu ya Televishen iilitolewa ikiwa na
Jina hilo hilo, katika TNT tarehe 07/02/2009, na kushinda tuzo ya Academi ya
Gooding jr ikiongozwa na Kimberly Elise akimwelezea mama yake.
Mwandishi; F.A.Maige.
Kuwa wa kwanza kupata info za matukio hapa.

0 comments:
Post a Comment