Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Featured Posts

Thursday, December 9, 2021

VIJANA TUJIFUNZE KWENYE UWEKEZAJI WA JUX

                JUX AONESHA DUKA LAKE JIPYA LA AFRICAN BOY STORE, AFANYA PARTY KULIZINDUA,  MASTAA WAHUDHURIA - YouTube 

Kipindi cha hapo nyuma  tulizoea kuona watu wenye mafanikio katika jamii yetu ni wa wanasiasa ,wafanyakazi wa serikalini na wafanya biashara wakubwa hivyo kila mzazi kutamani mtoto wake afanye kazi katika hizo nyanja.
 Ila hii ni tofauti kidogo na sasa kwani sanaa pia ni moja ya sehemu kubwa ambayo vijana wanajikwamua kiuchumi na kuendesha maisha yao ya kila kwa kupitia vipaji vyao ikiwemo muziki, uchekeshaji na utangazaji.
Hivi karibuni tumemshuhudia msanii wa Tanzania maarufu kwa uimbaji wa nyimbo za rnb juma jux akifanikiwa kufungua duka lake la mavazi ya brand yake ya African Boy, hakika ni moja ya hatua kubwa anayostahili kupongezwa kwa kuonyesha uthubutu mbele ya jamii inayomzunguka.

Kwani jina la African Boy lilianza kama jina la utani, ikiwa kama hashtag, na kuanza kuzalisha nguo kwa mawakala, mpaka sasa inapata ofisi maalumu kubwa na yenye mvuto inayopatikana na ya jiji la biashara na lenye umaarufu Afrika mashariki na kati namaanisha Dar es salaam; mbali na hapo jux alienda mbali na kutangaza nafasi za kazi katika brand yake hiyo na kutanua wingo kwa vijana wenye chachu ya mafanikio kwa kufungua mwanya wa fursa kwa vijana wa kitanzania.

Hii inaendelea kuwa ni miongoni mwa alama kubwa nchini Tanzania na kuendelea kudhihirisha kuwa sanaa ya muziki wa bongo fleva hapa nchini inalipa kwa kiasi chake katika namna yake na kufanya vijana wengi waliolala kimawazo kuamini kuwa inawezekana kujiajiri na sio kuisubiri serikali kuajiri.
Hongera Jux, Hongera African Boy
 
       Written by THEREAL_AMBROSS

Kwa habari za uhakika endelea kuiamini blog yetu

KILELE CHA 9 DECEMBER LEO UWANJA WA UHURU

 
Na. John Mapepele
Rais wa Jamhuri ya Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru leo Disemba 9, 2021 amesema Tanzania imepiga hatua kubwa kwenye lugha ya Kiswahili.

Rais Samia ameyasema haya jana usiku Disemba 8, 2021 jijini Dar es Salaam wakati akiwahutubia wananchi ambapo alieleza pamoja na mambo mengine mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 60 ya uhuru wa Tanzania.
 

“Nchi nyingi zinatumia lugha za kigeni kama lugha za mataifa yao zinazowaunganisha, inapendeza kuona kuwa tunatimiza miaka 60 tukiwa wamoja wenye utambulisho mmoja na lugha moja ya Kiswahili inayoendelea kupata umaarufu kimataifa   siku hadi siku”. Amefafanua Rais Samia.

Amesema wakati Tanzania ilipopata uhuru Kiswahili haikuwa lugha inayozungumzwa na watu wote ndani ya Tanganyika bali kizazi kilichofuata baada ya uhuru walijifunza kiswahili shuleni. Hii inafanya nchi kuwa kati ya nchi chache zenye lugha ya taifa yenye asili ya nchi husika.

Ameongeza kuwa katika miaka 60 Tanzania imefanikiwa kushawishi Kiswahili kuwa moja ya lugha rasmi zinazotumika  katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini  mwa Afrika na Umoja wa Afrika.
 

Amesema, Shirika la Umoja wa Mataifa Sayansi na Elimu (UNESCO) limepitisha azimio la kutenga siku ya tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani ambapo amesema azimio hilo linaifanya lugha ya Kiswahili kuwa kuwa ya kwanza katika bara la Afrika kutambuliwa na kutengewa siku yake rasmi.
 

Akiongea na Waandishi wa Habari hivi karibuni, mara baada ya UNESCO kupitisha rasmi azimio hilo Waziri mwenye dhamana ya Utamaduni nchini, Mhe. Innocent Bashungwa aliwataka wadau mbalimbali wa Kiswahili nchini kuendelea kutumia lugha hiyo ili iendelee kukua duniani.

Wednesday, December 1, 2021

RAIS WA ZANZIBAR DK. HUSSEIN MWINYI AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI.

 


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali akiwemo Meja Jenerali mstaafu Sharif Shehe Othman kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco).


Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Jumatano Desemba Mosi, 2021 na kusainia na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Zena Said imesema uteuzi huo unaanza leo.


Taarifa hiyo pia imemtaja Meja Jenerali mstaafu Said Shaaba Omar kwamba ameteuliwa kuwa mwenyeki wa bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma za Maji na Nishati, Zanzibar (Zura).


Mwingine aliyepata uteuzi ni Meja Jenerali mstaafu Issa Sleiman Nassor ambaye anakuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji, Zanzibar (Zawa).


“Said Haji Mdungi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa idara ya Nishati na Madini katika Wizara ya Maji, Nishati na Madini,” amesema

FAHAMU MASUALA YA UGONJWA WA MOYO.

 

UTANGULIZI – YAJUE MAGONJWA YA MOYO

Magonjwa ya Moyo ni magonjwa yanayoambatana na kuathiri moyo. Mara nyingi magonjwa ya moyo yanaambatana na mishipa ya damu kuwa na tatizo ambapo moyo hushindwa kufanya kazi, moyo hutegemea damu ambayo hubeba oxygen, madini, vitamins, kinga ya mwili, joto, homoni na vingine vingi.

Kwa mwaka 2015 pekee zaidi ya watu milioni 17.7 walifariki kutokana na magonjwa ya moyo na mfumo wa damu. Hii ni sawa na theluthi ya vifo vyote duniani. Zaidi ya theluthi ya vifo vyote vinavyotokana na ugonjwa wa moyo na mishipa ya damu hutokea ndani ya nchi zenye uchumi wa chini na uchumi wa kati

Different-Problems-of-the-Heart.

AINA ZA MAGONJWA YA MOYO

Zipo aina mbalimbali za magonjwa ya moyo hutofautiana japo yote huathiri moyo, nayo ni;

  1. Ugonjwa wa moyo unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu (Coronary artery disease) Hili ni tatizo linalowakuta watu wengi, mishipa ya damu hupasuka na kuharibika hii hutokana na mishipa ya damu kuwa na uchafu na mafuta mengi na kufanya damu isipite vizuri
  2. Mapigo ya moyo kwenda tofauti (Heart Arrhythmias) Hii hutokea pale mapigo ya moyo kwenda taratibu isivyo kawaida au kwenda haraka isivyo kawaisda, pia mapigo ya moyo kwenda ovyo. Hii ni hatari sana na huua sana
  3. Moyo kushindwa kufanya kazi (Heart Failure) Hii ni hali moyo hushindwa kufanya kazi yake kama kupampu na kusambaza damu, kusambaza oxygen. Hii inaweza kutokea kwa mtu mwenye magonjwa kama ugonjwa wa moyo wa misipa kuathirika, Shinikizo la damu, na magonjwa mengine
  4. Magonjwa ya moyo ya kuzaliwa (Congenital heart disease) Haya ni magonjwa ambayo wengi huzaliwa nayo, yanaweza kuwa ni baadhi ya kasoro katika mwili kama baadhi ya chemba za moyo kuziba au kupasuka, oxygen kupita kwa shida na vinginevyo.
  5. Ugonjwa wa valvu na misuli ya moyo (Heart Valve Disease & Cardiomyopathy (Heart Muscle Disease)) Katika moyo kuna chema nne nazo zinapitisha damu na  oxygen kutoka kwenye mapafu, valvu hufunguka na kufunga. Valvu na misuli ikiwa imepasuka na kuharibika husababisha tatizo la moyo.
  6. Moyo kutanuka. Hii hutokea pale damu ikiingia ndani ya moyo harafu mishipa ya kutoa damu ikiwa na tatizo ikashindwa kutoa damu nje ya moyo moyo utaanza kutanuka siku hadi siku. Kutanuka kwa moyo kunatokea usipotibu baadhi ya matatizo kama shinikizo la damu, moyo kwenda mbio, valvu na misuli ya moyo n.k.
  7. Shinikizo la damu (B.P) ni shinikizo la damu yako kwenye kuta za mishipa yako kwani moyo wako unasukuma karibu na mwili wako. Unaweza kuwa na shinikizo la damu (shinikizo la damu) kwa miaka bila dalili yoyote.
  8. Mshtuko/ Shambulio la moyo (Heart Attack). Ni kifo cha sehemu ya misuli ya moyo inayosababishwa na kuzuiwa wa usambazaji wa damu. Amana zilizo na mafuta huunda kwa wakati, na kutengeneza alama katika mishipa ya moyo wakoIkiwa baadhi ya misuli ya moyo inakufa, mtu hupata maumivu ya kifua na kukosekana kwa umeme kwa tishu za misuli ya moyo.
  9. Chembe ya Moyo. Hii ni maumivu ya upande wa moyo maeneo ya kifua hutokea wakati unafanya kazi au hata kama umekaa kama ni yenye kukubuhu. Maumivu haya huambatana na kutokwa jasho na kukosa hewa. Hutokana na moyo kukosa damu ya kutosha.

CHANZO CHA MAGONJWA YA MOYO

Magonjwa ya moyo hutokea pale ambapo moyo huathiriwa na kuharibiwa kwa vitenda kazi vyake. Kuna mitindo ya maisha inayoweza kukuweka hatarini kupata magonjwa ya moyo nayo ni pamoja na;

Heart-Disease
  1. Kuwa na halemu (Cholesterol) na Shinikizo la damu (B.P)
  2. Kuvuta sigala
  3. Uzito kupita kiasi na unene uliozidi
  4. Kisukari
  5. Kukaa sehemu kwa mda mrefu bila kuufanyisha kazi mwili
  6. Umri
  7. Ulaji holela wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi
  8. Utumiaji wa vinywaji vinavyobadili hali ya mwili
  9. Historia magonjwa yanayoambatana na moyo katika familia

DALILI ZA UGONJWA WA MOYO

Mara nyingi dalili hujionesha wakati mtu kakaa na ugonjwa kwa mda mrefu kidogo, ila kuna zingine zinatangulia na mara nyingi wengi huwa wanazipuuzia. Uonapo baadhi ya dalili fanya mawasiliano.

_f1a96da2-3a3a-11e8-8aa5-05fdb8d0ae52
  1. Moyo kwenda mbio (Moyo kudunda kwa nguvu isivyo kawaida )
  2. Uchovu uliopitiliza, mwili kuwa dhaifu na kuchoka haraka hata kwenye shughuri ndogo
  3. Maumivu ya kifua hasa yanayotembea mpaka kwenye mabega, shingo au taya
  4. Kushindwa kulala vizuri hasa kushtuka usingizini kuhisi kama unakabwa na kukosa pumzi
  5. Tumbo kujaa, kichefuchefu na kutapika
  6. Kukosa pumzi au kushindwa kupumua vizuri hasa unapolala chali
  7. Miguu, uso na tumbo kuvimba na kujaa maji

JINSI YA KUEPUKANA NA MAGONJWA YA MOYO

  1. Fanya mazoezi – Angalau dakika 30 kwa siku
  2. Usile vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi
  3. Usitumie chumvi mbichi au chumvi nyingi
  4. Punguza (balansi) kiwango cha halemu (choresterol)
  5. Balansi usito wako
  6. Usivute sigara
  7. Punguza au acha kunywa pombe
  8. Punguza mawazo
  9. Kula vizuri vyakula bora hasa asilia na sio vyakula vyenye kemikali
  10. Lala vizuri kwa muda mzuri – masaa 7 hadi 9

TIBA YA MAGONJWA YA MOYO

Magonjwa ya moyo yanatibika kwa hali tofauti, pia kufuatana na mda wa tatizo, mara nyingi wagonjwa wamekuwa wakikata tamaa na kuwa wabishi, hii hufanya wengi kufa kutokana na kuto kuwa makini na kile tunacho waeleza.

DAWA YA MAGONJWA YA MOYO

Tuna dawa ya kutibu kabisa magonjwa ya moyo ambayo ni ya asili isiyo na kemikali ambayo hufanya mtu kupona na kuimarika kabisa. : Dawa hiyo hutibu kulingana na mda wa tatizo, ukianza kutumia baada ya wiki moja MTU huanza kupona na kuonesha mabadiliko, pia mgonjwa anapewa mfumo wa maisha ambao inatakiwa autumie kwasababu kuna baadhi ya mitindo ya maisha inaendelea kuongeza tatizo pia kuna mitindo inapunguza hatari ya ugonjwa.

Tunamshukru Mungu kwa uumbaji wake na kutupa dawa ambazo alizileta ili kutuimarisha na kutuponya, Mungu hakuumba dawa nyingine zaidi ya mimea na vitu vingine vya asili, japo wengi hudharau. Mungu tunaomba utuokoe na kutuponya.

FAHAMU KWA KINA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME

 

UTANGULIZI – LIJUE TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Upungufu wa Nguvu za Kiume ni hali ya kushindwa kufanya mapenzi kikamililifu au kushindwa kusimamisha vizuri, shughuli ya tendo la ndoa huhusisha akili, homoni, neva, misuli, hisia na mirija ya damu. atizo hili huripotiwa kuwa katika wanaume watano (5) basi mmoja kati yao anatatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Upungufu wa nguvu za kiume huashiria kuto kuwa sawa kiafya hivyo ni tatizo linalohitaji tiba.

Hili tatizo huwanyima watu raha kwa kuwa na mawazo, kuwa na matatizo katika mahusiano, watu wengi wenye tatizo hili wanahitaji kutumia dawa zisizo na madhara na kubadilisha mitindo ya maisha yao ili kuweza kurudisha hali zao na kuondoa tatizo, cha msingi ni kuzingatia yale utakayoelekezwa.

Kuna matatizo ya kutofanya mapenzi kikamilifu, nayo ni; kuwahi kumwanga mbegu za uzazi, Kuto kumwaga, kutokuwa na hamu ya tendo la ndoamaxresdefault (1)

CHANZO CHA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Tatizo la nguvu za kiume lina vyanzo vingi ambavyo mara nyingi wengi huvipuuza, hivyo vyanzo huathiri taratibu na vingine huathiri haraka, tunashauri watu kuwa makini sana ili kujiimarisha vizuri. Kuna mitindo ya maisha inayoweza kukuweka hatarini kupata tatizo la nguvu za kiume nayo ni pamoja na;

  1. Kuwa na halemu (Cholesterol) na Shinikizo la damu (B.P) au ugonjwa wa moyo
  2. Kuvuta sigala na unywaji wa pombe
  3. Uzito kupita kiasi na unene uliozidi
  4. Ulaji holela wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi
  5. Kisukari
  6. Kuwa na mawazo na wasiwasi
  7. Matumizi ya madawa mbalimbali
  8. Umri hasa wazee
  9. Utumiaji wa vinywaji vinavyobadili hali ya mwili
  10. Kuwa na tatizo la kibofu
  11. Tabia za kujichua kwa mda mrefu
  12. Kutopata usingizi kamili
  13. Matumizi makubwa ya dawa zenye kemikali za kutibia magonjwa kama kansa, vidonda vya tumbo, moyo, kisukari, B.P, na magonjwa mengine

DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Dalili za kuonesha kuwa una tatizo la upungufu wa nguvu za kiume karibia zote zinahusiana na hali itakayo onekana katika tendo la ndoa au mda wa kujamiiana, hizo dalili zake ni kama;3850378299001_5085141251001_5085119722001-vs

  1. Kuwahi kufika kileleni
  2. Kukosa hamu ya mapenzi
  3. Kushindwa kurudia tendo la ndoa
  4. Uume kusimama kwa uregevu au kushindwa kusimamisha
  5. Kuchoka sana baada ya tendo la ndoa na hata kukinai kabisa au hata kusikia kichefuchefu; Miguu, uso na tumbo kuvimba na kujaa maji
  6. Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo hilo
  7. Kuchelewa sana kufika kileleni (au kushindwa kufika kileleni kabisa)
  8. Kukosa pumzi na uchangamfu wa mwili katika utendaji

JINSI YA KUEPUKANA NA KUPATA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME

  1. Fanya mazoezi – Angalau dakika 30 kwa siku
  2. Kula vyakula asilia na usile vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi
  3. Tibu magonjwa yako yanayokuweka hatarini kama kisukari, moyo, punguza unene na mengine
  4. Punguza (balansi) kiwango cha halemu (choresterol) au mafuta yaliyozidi
  5. Balansi usito wako
  6. Usivute sigara
  7. Punguza au acha kunywa pombe
  8. Punguza mawazo
  9. Kula vizuri vyakula bora hasa asilia na sio vyakula vyenye kemikali
  10. Lala vizuri kwa muda mzuri – masaa 7 hadi 9
  11. Usitumie dawa zenye kemikali nyingi huathiri mfumo wa uzazi
  12. Kunywa maji ya kutosha

TIBA YA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Hili ni tatizo ambalo huwanyima raha watu wengi kwasababu linaashiria upungufu flani wa kimwili, tunawashauri watu wengi wafanye mazoezi, kula chakula bora hasa asilia na pia wanywe maji mengi ili kuimarisha afya zao. Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume linaondolewa japo ni kwa mda mrefu kidogo, wengi hudanganywa na kupewa dawa za kuongeza nguvu pale unapoenda kujamiiana na sio dawa ya kutibu.

Tuna dawa ya kutibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume ambayo ni ya asili isiyo na kemikali ambayo hufanya mtu kupona na kuimarika kabisa. Dawa hiyo hutibu kwa mda  kulingana na ukubwa wa tatizo, ukianza kutumia baada ya wiki mbili huonesha mabadiliko, pia mgonjwa anapewa mfumo wa maisha ambao inatakiwa utumie kwasababu kuna mtindo wa maisha unaendekea kuongeza tatizo pia kuna mtindo unapunguza hatari ya ugonjwa.

Tunamshukru Mungu kwa uumbaji wake na kutupa dawa ambazo alizileta ili kutuimarisha na kutuponya, Mungu hakuumba dawa nyingine zaidi ya mimea na vitu vingine vya asili, japo wengi hudharau. Mungu tunaomba utuokoe na kutuponya.


LEO NI SIKU YA UKIMWI DUNIANI DEC 1

 Kwenye mji mkuu wa Dd'jamena Chad, mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 17 akitabasamu baada ya kupimwa na kubainika kuwa hana VVU.

Ikiwa leo ni siku ya Ukimwi duniani maudhui yakiwa kumaliza ukosefu wa usawa ili kila mtu aweze kupata huduma za kujikinga au kupunguza makali dhidi ya Virusi Vya Ukimwi, VVU na Ukimwi, shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, kanda ya Afrika limesema maudhui hayo yamekuja wakati muafaka kwa kuwa ukosefu wa usawa ndio chanzo cha kuibuka na kusambaa kwa magonjwa ya milipuko na yaliyojikita mizizi barani Afrika.
 

Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika Dkt. Matshidiso Moeti amesema kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa mshikamano wa kimataifa utasaidia kumaliza ukosefu wa usawa na hivyo kuhakikisha kila mtu anapata haki sawa za kibinadamu katika kujikinga na kutibiwa VVU na Ukimwi.

WHO inasema barani Afrika pekee, watu 1,300 hufariki dunia kila siku kutokana na magonjwa yanayohusiana na VVU na Ukimwi kwa hiyo “lazima tuhakikishe kila mtu, kokote aliko ana fursa sawa ya kinga dhidi ya VVU, kupata vipimo, tiba na huduma za matunzo ikiwemo chanjo pia dhidi ya COVID-19 na huduma nyinginezo muhimu.”

Takwimu zinaonesha kuwa asilimia 67 ya watu wote wanaoishi na VVU wako katika ukanda wa WHO barani Afrika.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na Ukimwi, UNAIDS linasema miaka 40 tangu mgonjwa wa kwanza wa Ukimwi aripotiwe duniani, bado VVU vinatishia ulimwengu.

Na kama hiyo hatoshi leo hii dunia haiko kwenye mwelekeo wa kufanikisha azma yake ya kutokomeza UKIMWI ifikapo mwaka 2030 si kwa sababu ya ukosefu wa ufahamu wa kile cha kufanya,  au ukosefu wa mbinu za kutokomeza UKIMWI, bali kwa sababu ya mifumo ya ukosefu wa usawa ambayo inazuia majawabu dhidi ya kinga na tiba kwa VVU kufikia kila mhitaji.

MESSI MCHEZAJI NDIO MCHEZAJI BORA WA MWAKA KWA MARA YA SABA BALLON D`OR

 

Mshambuliaji wa Paris St-Germain na Argentina Lionel Messi ameibuka mshindi wa taji la Ballon d'Or - linalokabidhiwa mchezaji bora wa soka wa mwaka kwa mara ya saba .

Messi aliisaidia nchi yake kushinda taji la Copa America , likiwa ndio taji lake la kwanza la kimataifa , na amefunga magoli 40 mwaka 2021 - 28 akiifungia Barcelona , manne akiifungia PSG na manane akiifungia Argentina.

Mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski alikuwa wa pili , huku kiungo wa kati wa Chelsea na Itali Jorginho akiwa wa tatu , naye mshambuliaji wa Real Madrid na Ufaransa Karim Benzema akiwa katika nafasi ya nne.

Taji hilo hupigiwa kura na waandishi 180 kutoka kote duniani , ijapokuwa hakukuwa na taji lililotolewa mwaka 2020 kutokana na mlipuko wa jangwa la corona.

Messi na Christiano Ronaldo walifanikiwa kushinda taji hilo mara tano kila mwaka kuanzia 2008, 2019 isipokuwa 2018 wakati kiungo wa kati wa Croatia Luka Modric alipotawazwa kuwa mshindi

Messi alikuwa tayari ashaibuka mshindi mara nyingi zaidi ya mchezaji mwengine yeyote baada ya kushinda mwaka 2009, 2010, 2012, 2015 na 2019.

"Ni furaha isio na kifani kuwa hapa tena ," alisema katika sherehe hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Paris wa Theatre du Chatelet.

"Miaka miwili iliopita nilidhani ndio mara ya mwisho. Watu walianza kuniuliza ni lini nitastaafu lakini sasa niko hapa Paris nikiwa na furaha''.

"Ni mwaka maalum kwangu na taji hili la Copa America , Iilikuwa na maana kubwa kushinda 1-0 dhidi ya Brazil katika fainali iliochezwa katika uwanja wa Maracana na nilifurahia sana kusherehekea na raia wa Argentina.

''Sijui iwapo ndio tuzo bora katika maisha yangu nimekuwa na kipindi kirefu cha mchezo - lakini ilikuwa tuzo muhimu pamoja na ile ya Argentina baada ya kupitia kipindi kigumu na changomoto chungu nzima na ukosoaji''.

Messi pia alikuwa na maneno matamu kwa mshambuliaji wa Bayern Roberto Lewandoski aliyechukua nafasi ya pili.

''Nilitaka kusema kwamba ni heshima kubwa kushindana na Robert'', alisema Messi. ''Alihitaji kushinda mwaka uliopita''.

Lewandowski alifunga magoli 53 katika mashindano yote 2021 akiichezea Bayern na alituzwa tuzo la mshambuliaji wa mwaka , tuzo mpya ambayo ilitangazwa saa chache kabla ya sherehe hiyo kuanza.

Kipa wa Paris St-Germain Gianluigi Donnarumma, ambaye aliisaidia Itali kushinda kombe la Euro 2020, alishinda taji la Yashin Trophy kwa kuwa kipa bora , huku klabu ya Chelsea ilioshinda taji la klabu bingwa Ulaya ikishinda tuzo ya klabu bora ya mwaka.

Kiungo wa kati wa Barcelona Pedri, 19, alishinda tuzo ya Kopa Trophy kwa kuwa mchezaji bora mwenye umri mdogo wa miaka ya chini miaka 21 , huku mchezaji wa England Jude Bellingham , Mason Greenwood na Bukayo Saka wakichukua nafasi ya pili ya tano na ya sita mtawalia.

Wachezaji 14 kati ya 30 walioorodheshwa kuwania taji la hilo kwa sasa wanachezea ligi ya Premia.

Chelsea ilikuwa na wachezaji watano , huku mchezaji aliyeibuka katika nafasi ya tatu Jorginho akijiunga na N'Golo Kante katika nafasi ya tano Romelu Lukaku katika nafasi 12, Mason Mount katika nafasi 19 na Cesar Azpilicueta, akiwa katika nafasi ya 29 .

Mabingwa wa ligi ya Premia Manchester City walikuwa na idadi sawa kupitia Kevin de Bruyne aliyemaliza wa nane , Raheem Sterling 15, Riyad Mahrez 20, Phil Foden 25 and Ruben Dias 26.

Wachezaji wawili wa Manchester United Ronaldo na Bruno Fernandes walimaliza katika nafasi ya sita na 21 mtawalia, huku mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah akimaliza katika nafasi ya 7 naye mshambuliaji wa Tottenham Hary Kane akimaliza katika nafasi ya 23.

Lionel Messi akishinda taji la Copa America

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Lionel Messi akishinda taji la Copa America

Matokeo ya Ballon d'Or

  • Lionel Messi (Paris St-Germain/Argentina, forward)
  • Robert Lewandowski (Bayern Munich/Poland, forward)
  • Jorginho (Chelsea/Italy, midfielder)
  • Karim Benzema (Real Madrid/France, forward)
  • N'Golo Kante (Chelsea/France, midfielder)
  • Cristiano Ronaldo (Manchester United/Portugal, forward)
  • Mohamed Salah (Liverpool/Egypt, forward)
  • Kevin de Bruyne (Manchester City/Belgium, midfielder)
  • Kylian Mbappe (Paris St-Germain/France, forward)
  • Gianluigi Donnarumma (Paris St-Germain/Italy, goalkeeper)
  • Erling Braut Haaland (Borussia Dortmund/Norway, forward)
  • Romelu Lukaku (Chelsea/Belgium, forward)
  • Giorgio Chiellini (Juventus/Italy, defender)
  • Leonardo Bonucci (Juventus/Italy, defender)
  • Raheem Sterling (Manchester City/England, forward)
  • Neymar (Paris St-Germain/Brazil, forward)
  • Luis Suarez (Atletico Madrid/Uruguay, forward)
  • Simon Kjaer (AC Milan/Denmark, defender)
  • Mason Mount (Chelsea/England, midfielder)
  • Riyad Mahrez (Manchester City/Algeria, forward)
  • Bruno Fernandes (Manchester United/Portugal, midfielder), tied with Lautauro Martinez (Inter Milan/Argentina, forward)
  • -
  • Harry Kane (Tottenham/England, forward)
  • Pedri (Barcelona/Spain, midfielder)
  • Phil Foden (Manchester City/England, forward)
  • Nicolo Barella (Inter Milan/Italy, midfielder), tied with Ruben Dias (Manchester City/Portugal, defender) and Gerard Moreno (Villarreal/Spain, forward)
  • -
  • -
  • Luka Modric (Real Madrid/Croatia, midfielder), tied with Cesar Azpilicueta (Chelsea/Spain, defender)
  • -
 
 
Blogger Templates