Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Wednesday, December 1, 2021

MESSI MCHEZAJI NDIO MCHEZAJI BORA WA MWAKA KWA MARA YA SABA BALLON D`OR

 

Mshambuliaji wa Paris St-Germain na Argentina Lionel Messi ameibuka mshindi wa taji la Ballon d'Or - linalokabidhiwa mchezaji bora wa soka wa mwaka kwa mara ya saba .

Messi aliisaidia nchi yake kushinda taji la Copa America , likiwa ndio taji lake la kwanza la kimataifa , na amefunga magoli 40 mwaka 2021 - 28 akiifungia Barcelona , manne akiifungia PSG na manane akiifungia Argentina.

Mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski alikuwa wa pili , huku kiungo wa kati wa Chelsea na Itali Jorginho akiwa wa tatu , naye mshambuliaji wa Real Madrid na Ufaransa Karim Benzema akiwa katika nafasi ya nne.

Taji hilo hupigiwa kura na waandishi 180 kutoka kote duniani , ijapokuwa hakukuwa na taji lililotolewa mwaka 2020 kutokana na mlipuko wa jangwa la corona.

Messi na Christiano Ronaldo walifanikiwa kushinda taji hilo mara tano kila mwaka kuanzia 2008, 2019 isipokuwa 2018 wakati kiungo wa kati wa Croatia Luka Modric alipotawazwa kuwa mshindi

Messi alikuwa tayari ashaibuka mshindi mara nyingi zaidi ya mchezaji mwengine yeyote baada ya kushinda mwaka 2009, 2010, 2012, 2015 na 2019.

"Ni furaha isio na kifani kuwa hapa tena ," alisema katika sherehe hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Paris wa Theatre du Chatelet.

"Miaka miwili iliopita nilidhani ndio mara ya mwisho. Watu walianza kuniuliza ni lini nitastaafu lakini sasa niko hapa Paris nikiwa na furaha''.

"Ni mwaka maalum kwangu na taji hili la Copa America , Iilikuwa na maana kubwa kushinda 1-0 dhidi ya Brazil katika fainali iliochezwa katika uwanja wa Maracana na nilifurahia sana kusherehekea na raia wa Argentina.

''Sijui iwapo ndio tuzo bora katika maisha yangu nimekuwa na kipindi kirefu cha mchezo - lakini ilikuwa tuzo muhimu pamoja na ile ya Argentina baada ya kupitia kipindi kigumu na changomoto chungu nzima na ukosoaji''.

Messi pia alikuwa na maneno matamu kwa mshambuliaji wa Bayern Roberto Lewandoski aliyechukua nafasi ya pili.

''Nilitaka kusema kwamba ni heshima kubwa kushindana na Robert'', alisema Messi. ''Alihitaji kushinda mwaka uliopita''.

Lewandowski alifunga magoli 53 katika mashindano yote 2021 akiichezea Bayern na alituzwa tuzo la mshambuliaji wa mwaka , tuzo mpya ambayo ilitangazwa saa chache kabla ya sherehe hiyo kuanza.

Kipa wa Paris St-Germain Gianluigi Donnarumma, ambaye aliisaidia Itali kushinda kombe la Euro 2020, alishinda taji la Yashin Trophy kwa kuwa kipa bora , huku klabu ya Chelsea ilioshinda taji la klabu bingwa Ulaya ikishinda tuzo ya klabu bora ya mwaka.

Kiungo wa kati wa Barcelona Pedri, 19, alishinda tuzo ya Kopa Trophy kwa kuwa mchezaji bora mwenye umri mdogo wa miaka ya chini miaka 21 , huku mchezaji wa England Jude Bellingham , Mason Greenwood na Bukayo Saka wakichukua nafasi ya pili ya tano na ya sita mtawalia.

Wachezaji 14 kati ya 30 walioorodheshwa kuwania taji la hilo kwa sasa wanachezea ligi ya Premia.

Chelsea ilikuwa na wachezaji watano , huku mchezaji aliyeibuka katika nafasi ya tatu Jorginho akijiunga na N'Golo Kante katika nafasi ya tano Romelu Lukaku katika nafasi 12, Mason Mount katika nafasi 19 na Cesar Azpilicueta, akiwa katika nafasi ya 29 .

Mabingwa wa ligi ya Premia Manchester City walikuwa na idadi sawa kupitia Kevin de Bruyne aliyemaliza wa nane , Raheem Sterling 15, Riyad Mahrez 20, Phil Foden 25 and Ruben Dias 26.

Wachezaji wawili wa Manchester United Ronaldo na Bruno Fernandes walimaliza katika nafasi ya sita na 21 mtawalia, huku mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah akimaliza katika nafasi ya 7 naye mshambuliaji wa Tottenham Hary Kane akimaliza katika nafasi ya 23.

Lionel Messi akishinda taji la Copa America

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Lionel Messi akishinda taji la Copa America

Matokeo ya Ballon d'Or

  • Lionel Messi (Paris St-Germain/Argentina, forward)
  • Robert Lewandowski (Bayern Munich/Poland, forward)
  • Jorginho (Chelsea/Italy, midfielder)
  • Karim Benzema (Real Madrid/France, forward)
  • N'Golo Kante (Chelsea/France, midfielder)
  • Cristiano Ronaldo (Manchester United/Portugal, forward)
  • Mohamed Salah (Liverpool/Egypt, forward)
  • Kevin de Bruyne (Manchester City/Belgium, midfielder)
  • Kylian Mbappe (Paris St-Germain/France, forward)
  • Gianluigi Donnarumma (Paris St-Germain/Italy, goalkeeper)
  • Erling Braut Haaland (Borussia Dortmund/Norway, forward)
  • Romelu Lukaku (Chelsea/Belgium, forward)
  • Giorgio Chiellini (Juventus/Italy, defender)
  • Leonardo Bonucci (Juventus/Italy, defender)
  • Raheem Sterling (Manchester City/England, forward)
  • Neymar (Paris St-Germain/Brazil, forward)
  • Luis Suarez (Atletico Madrid/Uruguay, forward)
  • Simon Kjaer (AC Milan/Denmark, defender)
  • Mason Mount (Chelsea/England, midfielder)
  • Riyad Mahrez (Manchester City/Algeria, forward)
  • Bruno Fernandes (Manchester United/Portugal, midfielder), tied with Lautauro Martinez (Inter Milan/Argentina, forward)
  • -
  • Harry Kane (Tottenham/England, forward)
  • Pedri (Barcelona/Spain, midfielder)
  • Phil Foden (Manchester City/England, forward)
  • Nicolo Barella (Inter Milan/Italy, midfielder), tied with Ruben Dias (Manchester City/Portugal, defender) and Gerard Moreno (Villarreal/Spain, forward)
  • -
  • -
  • Luka Modric (Real Madrid/Croatia, midfielder), tied with Cesar Azpilicueta (Chelsea/Spain, defender)
  • -

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates