Mbunge wa Muheza Hamis Mwinjuma @MwanaFA ameshiriki Ujenzi wa Shule ya Msingi Mlingoti inayohamishwa kutoka Kicheba B kwenda Kicheba A baada ya kutakiwa kuhamishwa ilipokuwa awali kupisha upanuzi wa Barabara ya Pangani - Mkuzi - Muheza - Kicheba - Maramba - Mwanyumba hadi Mkinga katika eneo la Kicheba.
Mbali na hio Mbunge @MwanaFA pia amefanikiwa kukamilisha ujenzi wa chumba cha Darasa ambapo Watoto wa Darasa la kwanza na la pili wameshaanza kukitumia ikiwa sambamba na matundu manne kati ya 8 ya vyoo yapo katika hatua ya umaliziaji.
Akizungumza baada ya kukamilika kwa hatua hizo Mh @MwanaFA amesema———“Leo tulikuwa tunaendelea na hatua za awali za ujenzi wa chumba cha pili, ambapo nimefanikiwa kuchangia mifuko 150 ya saruji kwenye ujenzi huu wa Shule na nimeahidi kuichangia zaidi kwa kadri ya mahitaji'
Kwenye hatua hio Mbunge @MwanaFa aliambatana na Diwani wa Kata ya Kicheba Bwana Hamisi Mkodingo na viongozi wengine wa Serikali ya Kijiji.

0 comments:
Post a Comment