Saturday, July 17, 2021
MANGE KIMAMBI ACHARUKIA VYOMBO VYA HABARI VISIVYOLIPA MISHARA WAFANYAKAZI.
Aisee kumbe ni media zooooote kasoro Azam Tv hawalipi mishahara au wanachelewesha miezi mingi.Clouds nayo ni bonge ya jipu. Hawalipi pia. Choice Fm ndo kabisaaaa.
Unaambiwa wanachofanya ni kwamba kila media house ina watangazaji wakubwa ambao wanaogopa kuwa lose hao ndo kidogo wanakuwa hawazinguliwi sana. Yani kwenye kampuni nzima unakuta kuna watu 5-10 tu ambao ndo hawazinguliwi.
Na magari wanapewa waendeshe tu ila ni gari ya kampuni, so zile gari zinatumika kuwafanya wasiondoke hata kama mtu anazinguliwa kwenye mshahara ila akifikiria kurudisha gari inabidi ajikaze tu.
Azam TV inabidi tuipigie makofi. Sijapata lalamiko hata moja la mishahara kutoka wafanyakazi wa Azam TV. Ila kwingine kote ni mayolodos. Yani wafanyakazi wanajishaua tu kwenye social media for absolutely nothing ila in real life unaambiwa wana njaaaaaaaaaaaa kushinda wewe unaewatamania kuwa wanafanyakazi sehemu flani.
Jamani mpaka ITV mnaambiwa ni jipu sugu.
Ila sielewi tatizo ni nini? Hizi media house zinajiendesha kwa hasara ama? I don’t understand. Why wanashindwa kulipa watu mishahara? I don’t get it maana mtu ulie nje una imagine hizi kampuni zinatengeza pesa ndefu kwa jinsi unavyoziona kwa macho ya nje kumbe ndani ni mabomu tupu, hakuna faida mpaka wanashindwa kulipa mishahara. I’m shocked kwa kweli.
Imagine leo tarehe 17 wafanyakazi wa EFM na wengine wa wasafi na wa ITV hawajalipwa hadi leo hii. Wengine wanadai pesa za miezi zaidi ya mitatu.
Naskia wengi walioondoka Azam wanajilaumu mnoooo. Maana walidanganyika na mishahara mikubwa kufika huko mishahara wanapokea kwa manati na kurudi Azam hawawezi. Jamani mliopo Azam tulizeni makalio hata kama mshahara sio mkubwa kivile ila ni bora huko kila mwezi unalipwa ontime. Otherwise fanya research ongea na wenzio waliohama kwanza wakwambie ukweli kama wanalipwa kila mwezi.
EFM ndo hawalipi kupitia bank anymore. Wanawalipa mikononi so wafanyakazi wanahisi hata makato yao hayaendi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment