Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Wednesday, December 1, 2021

RAIS WA ZANZIBAR DK. HUSSEIN MWINYI AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI.

 


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali akiwemo Meja Jenerali mstaafu Sharif Shehe Othman kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco).


Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Jumatano Desemba Mosi, 2021 na kusainia na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Zena Said imesema uteuzi huo unaanza leo.


Taarifa hiyo pia imemtaja Meja Jenerali mstaafu Said Shaaba Omar kwamba ameteuliwa kuwa mwenyeki wa bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma za Maji na Nishati, Zanzibar (Zura).


Mwingine aliyepata uteuzi ni Meja Jenerali mstaafu Issa Sleiman Nassor ambaye anakuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji, Zanzibar (Zawa).


“Said Haji Mdungi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa idara ya Nishati na Madini katika Wizara ya Maji, Nishati na Madini,” amesema

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates