Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Thursday, December 9, 2021

VIJANA TUJIFUNZE KWENYE UWEKEZAJI WA JUX

                JUX AONESHA DUKA LAKE JIPYA LA AFRICAN BOY STORE, AFANYA PARTY KULIZINDUA,  MASTAA WAHUDHURIA - YouTube 

Kipindi cha hapo nyuma  tulizoea kuona watu wenye mafanikio katika jamii yetu ni wa wanasiasa ,wafanyakazi wa serikalini na wafanya biashara wakubwa hivyo kila mzazi kutamani mtoto wake afanye kazi katika hizo nyanja.
 Ila hii ni tofauti kidogo na sasa kwani sanaa pia ni moja ya sehemu kubwa ambayo vijana wanajikwamua kiuchumi na kuendesha maisha yao ya kila kwa kupitia vipaji vyao ikiwemo muziki, uchekeshaji na utangazaji.
Hivi karibuni tumemshuhudia msanii wa Tanzania maarufu kwa uimbaji wa nyimbo za rnb juma jux akifanikiwa kufungua duka lake la mavazi ya brand yake ya African Boy, hakika ni moja ya hatua kubwa anayostahili kupongezwa kwa kuonyesha uthubutu mbele ya jamii inayomzunguka.

Kwani jina la African Boy lilianza kama jina la utani, ikiwa kama hashtag, na kuanza kuzalisha nguo kwa mawakala, mpaka sasa inapata ofisi maalumu kubwa na yenye mvuto inayopatikana na ya jiji la biashara na lenye umaarufu Afrika mashariki na kati namaanisha Dar es salaam; mbali na hapo jux alienda mbali na kutangaza nafasi za kazi katika brand yake hiyo na kutanua wingo kwa vijana wenye chachu ya mafanikio kwa kufungua mwanya wa fursa kwa vijana wa kitanzania.

Hii inaendelea kuwa ni miongoni mwa alama kubwa nchini Tanzania na kuendelea kudhihirisha kuwa sanaa ya muziki wa bongo fleva hapa nchini inalipa kwa kiasi chake katika namna yake na kufanya vijana wengi waliolala kimawazo kuamini kuwa inawezekana kujiajiri na sio kuisubiri serikali kuajiri.
Hongera Jux, Hongera African Boy
 
       Written by THEREAL_AMBROSS

Kwa habari za uhakika endelea kuiamini blog yetu

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates