Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Sunday, July 11, 2021

DADARAO; KIFO CHA MWANAE CHAMPA UZALENDO INDIA.

Wazalendo wengi wamesikika lakini jina linguine la mzalendo limezaliwa na kuchukua sura mpya nchini India ,katika mji wenye purukushani nyingi na muingiliano wa wageni nchini humo maarufu kwa jina la Mumbai. Mwaka 2018 july 30 majira ya saa 9:50 Am katika makutano ya mataa mjini humo kulitokea ajali mbaya iliyosababishwa na mashimo katika barabara hiyo na kufanya piki piki aliyokuwa anaendesha binti mmoja mwenye umri wa miaka 16 ilikosa muelekeo na kuingia ndani ya uvungu wa gari hiyo na kusababisha kifo kwa binti huyo. Baada ya familia ya Mr. Dadarao bihore kupokea taarifa hyo kuhusu kifo cha binti yao walihuzunika na kumshukuru mungu waliamini ya kuwa tukio hilo ni mipango ya mung una sio uzembe wa dereva kama wengi walisikika wakisema, tangu mwaka huo mpaka hii leo familia ya Dadarao ilichukua hatua ya kurekebisha mashimo yaliyopo kwenye barabara za mji huo wa Mumbai kwa

gharama zao binafsi na mara kadhaa wanaandishi wa Habari walionekana kumzonga bwana Dadaro na kujaribu kumhoji ni kwa amehamua kufanya kazi hiyo ya kuziba mashimo yaliyomo kwenye barabara wakati hiyo kazi ilitakiwa ifanywe na serikali au viongozi husika lakini jibu lilikuwa tofauti kwa upande nukuu ``Nimejifunza mambo mengi tangu kitokee kifo cha binti yang una nimegundua familia nyingi hapa Mumbai zinapoteza watu wazima kwa Watoto kutokana na mashimo haya tukingojea mpaka serikali ije kufanya marekebisho tutaenedea kupoteza watu tunao wapenda.’’ Mpaka sasa imepita miaka 3 na miezi kadhaa tangu bwana Dadarao kumpoteza mtoto wake wa kike kipenzi, kwa juhudi zake na familia yake wamefanikiwa kurekebisha mashimo 556 kwa gharama zao. Serikali ya India na viongozi wake kwa ujumla wamevutiwa sana na uzalendo wa Dadarao kwa hatua hiyo imehamua kumuunga mkono mzalendo huyo na kuhaidi kufanya marekebisho katika barabara zote zinazopatikana katika nchi ya India.

              Mwandishi; F.A.Maige. 
 Kuwa wa kwanza kusoma matukio na habari hapa kwenye blog yetu.Asante.

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates