![]() |
Wengi kati yenu mnapenda kumuita Michelle Obama siyo kama mnakosea hapana lakini haya ndio majina aliyopewa baada tu ya kuzaliwa na kuuona uso wa dunia, jina la kuzaliwa ni Michelle LaVaughn Robinson), amezaliwa mnamo tar. 17 Januari 1964) ni Mwanasheria wa Kimarekani na ndiyo mke wa Rais mstaafu wa awamu ya 44 wa Marekani Bw. Barack Obama. Huyu ndiye Mwafrika Mwamerika wakwanza kuwa Mwanamke wa Kwanza wa Marekani.
Michelle alizaliwa
na kukulia katika kitongoji cha South Side ya Chicago na
kusoma hadi kuelekea katika Chuo Kikuu cha Princeton halafu
baadaye katika Kitivo cha
Sheria cha Harvard.
Baada ya kumaliza
elimu yake hiyo, alirudi Chicago na kukubali kuchukua nafasi ya kazi katika
kampuni ya Sidley Austin, halafu baadaye akaja kuwa kama mmoja kati ya
wafanyakazi wa meya wa Chicago Bw. Richard M. Daley, halafu baadaye akafanya
kazi katika Chuo Kikuu cha Chicago na
Hospitali za Chuo Kikuu cha Chicago.
Michelle Obama ni
dada wa Craig Robinson, kocha wa mpira wa kikapu wa Oregon State University.
Alikutana na Barack pale alipojiunga na Sidley Austin. Pale Barack Obama
alipochaguliwa kuwa kama Seneta, familia ya Obama ikachagua kuishi mjini
Chicago South Side kuliko kuishi mjini .Washington
D.C.Kati ya ndoto kubwa ya Michelle alitamani sana kuja kuolewa na mwanaume mwenye
ndoto za kuja kuwa Raisi wa marekani, kwa kuwa mungu hamtupi mja wake ndoto
hiyo ya Michelle ilitimia mwaka 2008 baada ya Obama kutangazwa ndio Raisi wa 44
kupitia chama cha Democratic.
Mwandishi; F.A.Maige.
Usisahau kupita kwenye blog yetu pendwa kila siku kusoma habari na matukio ya siasa na burudani kwa maoni na ushauri weka maoni yako.Asante

0 comments:
Post a Comment