Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Friday, October 22, 2021

ALEC BALDWIN AMEUUA MWANAMKE WAKATI WA KUTENGEZA FILAMU.


 Nyota wa sinema za Hollywood Alec Baldwin ameua mwanamke mmoja na kumjeruhi mwanaume kimakosa alipofyatua bunduki ya maigizo wakati wa kutengezwa filamu huko New Mexico.



Mwanamke huyo ametajwa kama Halyna Hutchins, 42, ambaye alikuwa akifanya kazi kama mkurugenzi wa upigaji picha.


Mtu anayetibiwa ni Joel Souza, 48, mkurugenzi wa filamu.


Polisi katika jimbo hilo la Marekani walisema Bw. Baldwin alitoa silaha hiyo wakati wa utengezaji wa filamu yake.


Msemaji wa Bw Baldwin aliliambia shirika la habari la AP kwamba kisa hicho kilihusisha utumiaji mbaya wa bunduki ya maigizo.


Polisi bado wanachunguza tukio hilo huko Bonanza Creek Ranch, eneo maarufu la utengenezaji wa sinema, na hakuna mashtaka yoyote yaliyofunguliwa dhidi yake.

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates