Kwenye mahusiano kuna kitu kinaitwa "Over reactivity". Hii ni ile hali ya mtu kuzidiwa na hisia za hasira kiasi cha kusema lolote au kufanya lolote bila kujali nini kitatokea.Hakuna ndoa isiyokuwa na changamoto kila ndoa ina changamoto zake, namna nzuri ya kukabili changamoto zinazo wakabili ndio tiba ya changamoto hizo. Jitahidi hata kama utakwazwa na mwenza wako kwa kiwango gani basi kuwa chini na vumilia ili usije kufika kwenye hali hii ya Over reactivity.
Hisia hizi za hasira zikishapewa nafasi kubwa ndani ya moyo basi hakuna kinachotokea zaidi ya uharibifu. Kwasababu hali hii ndio itamsukuma mtu kutukana bila kujali na hata kupigana pasi na woga. Matusi hayajawahi kuwa na tiba hata siku moja toka dunia iwe hai.
Kitu pekee kitakachomfanya mwenza wako kuwa mpya ni wewe kuvumilia kasoro za mwenza wako na kutafuta njia za busara katika utatuzi wa kasoro hizo. Kukasirika kiasi cha kumwaga matusi na kashfa hadharani hakujawahi kuwa tiba ya tatizo toka dunia iumbwe.
Kila kitu kinaweza kwenda sawa kama tukiishi kwenye kanuni vyema. Mara zote mihemko na kutunza makosa kwenye nafsi zetu ndio kitu pekee kinachoamsha hisia za chuki kiasi cha kufanya maamuzi magumu kwenye maisha yetu. Jitahidi kuishinda hali hii ya Over reactivity utafaulu sana maishani.

0 comments:
Post a Comment