TUKIO LA KWANZAMchezo kati ya Gwambina VS Simba mechi iliisha kwa simba kupata ushindi wa goli moja Mimi naliita goli kali la msimu kutoka kwa @official_mohamedhussein15 lakini baadaye simba walipata kona baada ya Mlinda mlango wa gwambina Mohamed Makaka kuokoa Shuti kali la Chama dakika ya 74 ya mchezo, kona inapigwa na Chama mpira ukatua kwa Onyango naye akaweka wavuni kwa kichwa lakini line one anakataa goli.
Kwa tukio hilo wengi tulitegemea @azamtvtz kupitia camera zao zilizopo karibu na tukio wangeweza kutuonyesha kwa karibu kabla, wakati wa kupigwa na baada ya mpira kupigwa nini kilitokea hadi line one aseme sio goli halali, hapo tulibakia na kigugumizi huku tukiaminishwa kuwa ule mpira ulitoka nje ya uwanja kabla haujamfikia mfungaji wa goli lakini baadaye ilipatikana video clip iliyorekodiwa na mtazamaji aliyekuwa karibu na eneo la kupigia kona iliyoonyesha kuwa mpira ule haukuwa umetoka nje ya uwanja wakati Mchezaji Chama ameupiga hivyo simba walinyimwa goli halali.
Najua kwamba hata kama Azam wangetuonyesha tukio hilo kwa usahihi lisingebadili matokeo lakini ingesaidia sana kuonyesha mapungufu ya waamuzi wetu.
TUKIO LA PILI.
Kwenye mchezo kati ya Namungo dhidi ya yanga uliochezwa Majaliwa Stadium napo kuna utata ulitokea dakika ya 73 na sekunde 40 alikuwa ni Saidoo alichonga kona ikamfikia (yacouba)akaweka kwenye wavu kwa bichwa matata sana lakini line one akainua Kibendera kwamba halikuwa goli, watazamaji tulitegemea kuona Azam TV watatuonyesha kwenye picha za majereo kwa kamera zilizokuwa zinachukua kwenye eneo la 18 kwa angle mbali mbalimbali ili tujiridhishe kwamba ni kweli Mwamnyeto aliotea au nao mpira ulitoka kwanza nje lakini hatukupata jibu na mechi iliisha bila bila kibaya zaidi kwenye mechi hii hatukupata clip yoyote kutoka kwa mashabiki.
Ushauri wangu natambua na ninapongeza sana jitihada zenu za kuinua Soka letu la Tanzania naomba nguvu ziongezwe Kwenye vifaa hasa kamera kwenye viwanja vya mikoani maana tatizo hilo ni nadra kwenye michezo inayochezwa viwanja vya Dsm.

0 comments:
Post a Comment