Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Monday, October 18, 2021

USIMDHARAU ANAEKUPENDA KWA DHATI.


Kupendwa ni tunu kubwa sana maishani, na sio wote wanapata bahati hiyo maishani mwao.


Aliekupenda kwa dhati lazima umthamini kwa haki kwasababu jambo aliolifanya kwako la upendo ni wazi kuwa amekupa hadhi ya juu na maana safi ya utu maishani mwako.

Ukitaka kujua kuwa upendo ni tunu kwako tizama nyumba zenye migogoro ya ndoa namna upendo unavyowakosesha usingizi kiza kiingiapo.

Nyumba yoyote ambayo afya ya upendo imepotea ni ngumu nyumba hiyo kuwa na amani hata ikiwa chini ya wasuruhishi wa kimataifa. Kwasababu upendo ndio bustani ya ridhaa kwenye nyumba ya mke na mume.

Kwenye upendo ridhaa huja na kwenye ridhaa upendo huwa umeshatangulia kamwe hakuna amani bila upendo kutokea. Pesa na mali haziwezi kuleta amani kwenye nafsi zisizokuwa na mapenzi ya dhati.

Hakikisha unatafuta mtu mwenye upendo wa dhati kwako haijalishi ni masikini au tajiri kubwa ni kupata ponyo la hisia na sio furahisho la tumbo na jicho.

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates