Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Tuesday, September 7, 2021

MWANAUME HAUDUMIWI ANAHUDUMIA.

 


 Ndoto ya kila mwanaume mvivu ni kupata mwanamke mwenye kipato kizuri, kwasababu ubora wa kipato cha mwanamke utamfanya yeye kukwepa majukumu yake kwa mkewe.


Mwanaume anaekimbia majukumu yake huyo sio mwanaume kamili bali ni mvulana ambae hajapevuka kiakili. Unapokubali kuoa maana yake umejikubalisha kusimamia stahiki zote za mwanamke kwako.

Kujisifu kuwa mkeo anakupenda sana na anakuhudumia hayo ni mawazo ya kisichana anaekaribia kukua. Mwanaume kamili anatafuta ili mkewe ale sio anatafutaiwa ili yeye ale. Fanya kazi brother umeumbwa ili uhudumie sio uhudumiwe.

Uwanaume sio upana wa misuli na six pack za kulipiwa Gym na mwanamke. Uwanaume ni ukubwa wa fikra na kujitumaili kutatua changamoto zinazowakabili watu wanaokuzunguka.

Bora ufuge kitambia ukiwa unatekeleza majukumu yako ipasavyo kwa mkeo kuliko kutuna misuli kwa pesa ambayo jasho katoa mkeo. Tafuta hela brother ili usimamie vyema majukumu yako. Six pack without money is nothing.

Hela itakufanya kuitwa baba bora. Hela itakufanya kuheshimiwa sehemu uliyodharaulika. Hela itakusogeza na watu bora wenye mawazo chanya kuhusu hela. Huwezi kuwa na hela kama hutafuti hela. Mwanaume kamili hachoki kujituma kwa ajili ya familia yake.

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates