Wanawake wilaya ya Handeni Mkoani Tanga wamemuomba Mkuu wa Wilaya Siriel Mchembe apaze sauti kwa niaba yao dhidi ya Wanaume wanaonyonya maziwa ya Wake zao kwa madai kuwa yanawaongezea nguvu za kiume.DC Mchembe ameikemea tabia hiyo na kuwataka Wanaume waache mara moja na kuongeza kuwa tabia hiyo inawakosesha watoto maziwa ya Mama, na kuwaweka hatarini kupata magonjwa
Kama tunavyofahamu kuhusu afya ya mama na mtoto ni salama pale wanapopata matunzo bora kwa wakati wote wa malezi, lakini kwa kipindi hiki imeonekana baadhi ya wababa hasa wa mikoani kuamini ya kuwa ukinyonya maziwa ya wake zao baada ya kujifungua kwa imani ya kuongeza madini mwilini.
Wewe msomaji wa blog hii pendwa una maoni gani kuhusu tamko hili...??

0 comments:
Post a Comment