Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Tuesday, August 24, 2021

SULEIMANI KOVA AFUNGUKA KUHUSU ASKOFU JOSEPHAT GWAJIMA KUOMBA KUBADILISHA KITI NA MICROPHONE.


 Kamanda Mstaafu Kanda Maalum ya Dar es saalaam Kamishna Suleiman Kova leo kwenye Amplifaya ya @CloudsFMTZ ameelezea tukio la Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima kuomba kubadilisha kiti na microphone vilivyokua vimeandaliwa kwa ajili yake kuvitumia wakati akihojiwa na Kamati ya Bunge Dodoma, Kova ameelezea tukio kama hili kwa kutumia uzoefu wake akiwa Polisi na kuhoji Watu mbalimbali wenye tuhuma.


"Wakati mwingine Mtu akishafanya jambo flani anakuwa na hisia flani ambazo sio za kawaida labda anafikiri nikikaa hapa naweza nikadhurika, ni tatizo la kisaikolojia kwa Mtu ambae ana msongo wa mawazo anakuwa hajiamini na haamini Mtu yeyote yule, kwahiyo anaweza kufanya jambo lolote lile”

"Mfano mimi zamani nilikua nahoji Wahalifu, akiletwa kwangu akisikia ni Kova anapoingizwa mule ndani anadondoka chini paap bila kumgusa, yani anaona amekutana na kitu cha hatari sana kutokana na yeye anavyoelewa, kama ni madhambi anayakumbuka yote" ——— Kamanda Mstaafu Kanda Maalum Dar es salaam Kamishna Suleiman Kova.

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates