Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Tuesday, August 24, 2021

FAMILIA YA MAREHEMU NIPSEY HUSSLE IMEKANUSHA MADAI YA MWANADADA KUHUSU WIMBO WA HUSSLE & MOTIVATE.

 


Familia ya marehemu Nipsey Hussle imekanusha madai ya mwanadada mmoja aitwaye Tasleema Yasin ambaye aliibuka na kudai kwamba anadai pesa za mirabaha baada ya sauti yake kutumika kwenye wimbo wa Hussle & Motivate.


Kwenye madai yake, Yasin amesema aliimba kiitikio cha wimbo huo uliopo kwenye album ya "Victory Lap" na pia kushiriki kwenye kuuandika. Lakini hakutaka sauti yake itumike kwenye Kolabo hiyo, Nipsey alienda kinyume na makubaliano na vile vile akashindwa kumtaja (credit) kama mshiriki kwenye wimbo huo.

Sasa mtandao wa RadarOnline umeripoti kwamba Blacc Sam ambaye ni Kaka wa Nipsey Hussle amefungua shauri akikanusha madai hayo ya mwanadada Yasin. Kwa mujibu wa tovuti hiyo, Sam hajataja sababu za kukanusha madai hayo.

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates