Wednesday, August 11, 2021
MSUMARI WA MWISHO WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KUHUSU SAKATA LA TOZO ZA SIMU:
Rais Samia Apigilia Msumari wa Mwisho Sakata la Tozo Kwenye SimuRais wa awamu ya sita wa Tanzania Samia Suluhu Hassani amesema serikali inawashukuru wananchi kwa kukubari kuchangishana kwa ajili ya tozo kwenye miamala ya simu.
Rais Samia amesema wananchi wamekuwa wakilalamila juu ya kiwango cha makato na sio tozo kam watu wengi wanavyoripoti na serikali imeleta sera hiyo ili kusaidia.
“Lalamiko kubwa la wananchi ilikuwa kiasi cha makato kinachoweka kwenye tozo wamekubari kuchanga na nashukuru kwenye hilo, maan tunataka tujenge vituo vya afya vingi, tunawabana wananchi kwa faida yao kila mtu ametoka kwenye hali ngumu hivyo tukichangishana inakuwa kwa faida yao”
Hii inakuwa ni mara ya pili kwa Rais Samia kusisitiza kuwa tozo hizo zinafaida kubwa kwa wananchi licha ya malalamiko kadhaa ya wananchi kuhusu tozo hizo
Je umezikubali tozo kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu? Toa maoni yako hapa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment