Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Monday, August 23, 2021

MBUNGE WA KAWE ASKOFU GWAJIMA AMEITIKIA WITO WA MBUNGE LEO MJINI DODOMA.


Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima leo Agosti 23 ametii wito kufika mbele Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge jijini Dodoma, ili kujibu tuhuma mbalimbali ikiwemo kusema uongo na kushusha hadhi na heshima ya bunge.


Gwajima ambaye ni Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, amewasili Viwanja vya Bunge Majira ya saa 6:40 mchana huu kuitikia wito wa kamati hiyo kufuatia wito wa Spika wa Bunge, Job Ndugai aliyemtaka mbunge huyo pamoja na Mbunge mwenzake, Jerry Slaa wa Ukonga kufika mbele ya kamati.

Gwajima amekuwa na msimamo wa kupinga chanjo ya corona na kusema waziwazi kuwa yeye na familia yake hawatochanjwa chanjo hiyo hata kama Bunge likilazimisha, hatochanjwa.


0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates