Saturday, August 28, 2021
ANJELA: NASTAHILI VIZURI ZAIDI KWA SASA NI MUDA WANGU.
Baada ya mapema wiki hii mrembo Anjella wa Konge Gang kuposti video ikiyomuonesha ameshika cheni ya silva yenye jina lake, hatimaye mwenyewe amefunguka kuwa kwa sasa anastahili vitu vizuri zaidi ya cheni hiyo.
Akizungumza Anjela @anjella_tz anasema kuwa, gharama za cheni hiyo ni shilingi milioni saba, lakini bado anaona kama anastahili kuwa na dhahabu za bei mbaya zaidi.
“Kwanza namshukuru bosi wangu, Harmonize kila siku kwa sababu yeye ndiye amefanya leo hii mimi niwe hapa.
“Cheni hii imegharimu shilingi milioni saba tu, lakini naona kabisa nastahili vitu vingine vizuri zaidi kwa sababu nafanya muziki mzuri na mashabiki wangu wanafurahi,” anasema Anjella.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment