Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Monday, July 12, 2021

ZANZIBAR; WAHUDUMU WA AFYA WAANZA KUPOKEA CHANJO YA COVID-19 KUTOKA CHINA.


 

Wahudumu wa afya visiwani Zanzibar wameanza kupokea dozi ya kwanza ya chanjo ya covid-19.Serikali ya Zanzibar imethibitisha kuwa dozi za Sinocav kutoka nchini China zimeanza kutolewa kwa awamu ya kwanza huku awamu ya pili ikitarajiwa kufanyika baada ya wiki mbili kutoka sasa.

‘’Tumeanza kutoa chanjo wiki iliyopita kwa wahudumu wetu wa afya, tunawapa chanjo ya Sinovac kutoka China ambayo imepitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Tuna wahudumu wa afya elfu sita lakini kwa sasa tutaanza na nusu yao,’’ Katibu wa wizara ya Afya Zanzibar Dkt Omary Dadi Shajak ameieleza BBC.

Kwa mujibu wa Dkt Shajak chanjo hiyo awali ilipangwa kutolewa kwa mahujaji waliokua waende Makka, lakini kutokana na kuzuiwa kwa mahujaji kutoka nje ya Saudi Arabia, Wizara hiyo imeamua kutumia chanjo kwa wahudumu wa Afya.

Mpango huo wa chanjo hata hivyo unawalenga wahudumu wa afya wa Zanzibar pekee. Dkt. Shajak ameongeza pia chanjo ya pamoja na Tanzania bara itatolewa kwa utaratibu maalum kupitia mpango wa Covax.

 

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates