Wednesday, July 28, 2021
STEVE NYERERE ATOA HUSIA MZITO KWA MANARA.
Rafiki inatosha kusema kila jambo lina Mwanzo na mwisho, Umefanya makubwa kwenye Simba, Hakuna mashabiki wa Simba wasiojua ulicho kifanya Ulijitoa kwa Moyo wako wote, Sio rahisi sana watu wote kujua uliyokuwa unapitia lakini kama akijua mwenyezi Mungu na family yako Inakupasa kusema Asante, @hajismanara Unakwenda kupumzika ukiwa umejenga uwezo mkubwa kwenye Mpira, Wewe ni Binadamu lazima kwa nafasi uliyokuwa nayo Maadui ni wengi kuliko watu wema Pokea na sema asante kwa kila jambo, Uzuri wako hujawahi kubagua rafiki kwa kuchagua uyu Yanga uyu mtibwa, uyu lipuli, Ulisimama na kusimamia kile unacho kiamini,Huwezi jua mbele ya safari Mungu anamipango gani na wewe ,Shukuru sema asante, Mara nyingi wanao fanya vizuri sana kwenye kila sekta basi huwa na maadui kila kona wa kumzalilisha na wengine wanatoka chumbani humo humo, Shika lile neno Isiwe Tabu, Tanguliza kila lenye mwanzo halikosi kuwa na Mwisho na maliza kwa kusema SHUJAAAAA hana thamani kwao, Unabaki kwenye midomo ya watu, Utaishi kwenye mifano mingi kwenye kila jambo la Simba, Utakumbukwa na Matokeo, Pumzika Mdogo wangu rafiki yangu kipenzi Haina shida tuna kesho nyingi kuliko Leo 1,THIS IS SIMBA WAACHIE USIONDIKE NAYO, WEWE SEPA NA BUGATI,
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment