Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Wednesday, July 28, 2021

SIMBA INAPASWA KUANZA KUFIKIRI MBADALA WA ONYANGO NA WAWA.

 

                                                    
Simba ndio timu bora zaidi nchini kwa sasa. Hilo halina ubishi hata kidogo. Timu yao imekamilika kweli kweli. Inavutia sana..
.
Haishangazi kuona imetwaa mataji manne mfululizo ya VPL.. Wametwaa mataji mawili mfululizo ya ASFC na wamefika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mara mbili katika miaka mitatu..
.
Wako vizuri.. Timu yao imekamilika kila idara... Kipa makini.. Mabeki katili na washambuliaji wenye njaa ya magoli... Halafu katikati mafundi kibao wa kuupaka mpira rangi.. Wataalam wa pasi za magoli.. Halafu wana Luis Miquissone mmoja..
.
Hata hivyo pamoja na yote, Simba inapaswa kuanza kutafuta mbadala wa mabeki wake, Pascal Wawa na Joash Onyango.. Tena wanapaswa kuanza kutafuta mapema.
.
Januari Mosi mwakani Wawa anafikisha miaka 36... Ni mingi sana.. Hasa kwa mchezaji wa kiafrika... Kwa sasa ndiye mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi pale Simba (kwa mujibu wa passport zao)..
.
Onyango naye anaonekana umri umesogea.. Mwili wake umeanza kuwa mzito.. Siyo mshapu tena sana katika kufanya maamuzi. Bila shaka hana muda mrefu kuendelea kucheza katika ubora wake..
.
Wakati Wawa na Onyango umri ukianza kuwawashia taa nyekundu, beki mwingine pia Erasto Nyoni naye umri unasonga.. Ni miongoni mwa wachezaji wakongwe zaidi nchini kwa sasa.. Anacheza ngazi ya Ligi Kuu kwa miaka 18 sasa..
.
Angalau Simba wana Ibrahim Ame na Kennedy Juma kama warithi wa Nyoni.. Inavutia kidogo.. Nasikia pia wanataka kumchukua Abdulmajid Mangalo wa Biashara United..
.
Ila yote kwa yote, Simba ianze kutazama mabeki mbadala wa Wawa na Onyango.. Kama siyo msimu huu, basi kwa msimu ujao..


0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates