Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Wednesday, July 28, 2021

RIPOTI KUHUSU UCHUNGUZI WA SOKO LA KARIAKOO WAKADHIWA KWA MAJALIWA.


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jana, July 27, 2021 amepokea taarifa ya Kamati ya Uchunguzi wa tukio la moto uliyotokea katika Soko la Kimataifa la Kariakoo July 10, 2021 jijini Dar es salaam.


Majaliwa amepokea taarifa hiyo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, CP Liberati Sabas na kuahihidi kuwa Serikali itayafanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolewa na Kamati hiyo.

Akizungumza baada ya kuipokea taarifa hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam, Majaliwa amewashukuru na amewapongeza Wajumbe wa Tume hiyo kwa kazi nzuri iliyofanyika kwa weledi mkubwa.

Majaliwa amesema ataifikisha taarifa hiyo kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwani tukio hilo limewagusa watu ndani na nje ya Nchi———“Naahidi mbele yako Mwenyekiti kuwa Serikali nimeridhishwa na taarifa mliyo nikabidhi leo na mapendekezo yote mliyoyatoa yatazingatiwa”

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates