Kanye West amekutana na Kevin Durant pamoja na Justin LaBoy jana mjini Las Vegas, awasikilizisha album yake mpya #DONDA ambayo inatajwa kuachiwa wiki hii. Kwa mujibu wa LaBoy ambaye masikio yake yamepata bahati hiyo, amesema hii itakuwa album ya mwaka kwani Kanye ameonesha mabadiliko makubwa kwenye muziki wake.-
"Kanye ametusikilizisha album yake mpya mimi na Kevin Durant, production yake ipo mbele ya muda, na mistari inasikika kama mtu mwenye njaa akitaka kusainiwa tena. Msanii yeyote ambaye amepanga kuachia kazi yake hivi karibuni, inabidi aisogeze mbele tu." aliandika Justin LaBoy.
Wikendi iliyopita ilivuja tracklist yenye jumla ya ngoma 9 zikiwa na jina la album, DONDA ambayo ni album ya 10 kwa Kanye West.

0 comments:
Post a Comment