Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa Tsh. MILIONI 100 kwa ajili ya ujenzi wa paa la kisasa la kuzuia jua na mvua kwa Wahanga 1,800 wa soko la Kariakoo waliohamishiwa Machinga Complex.Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amethibitisha kupokea fedha hizo wakati akizungumza na Wafanyabiashara hao.
RC Makalla amesema baada ya jana (July 20) kuwatembelea na kuwasikiliza, Rais Samia aliona changamoto hiyo na alipomuuliza (RC Makalla) kiasi cha fedha kinachohitajika alisema ni Milioni 62 za ujenzi wa paa la turubai lakini kwa kutambua umuhimu wa Wafanyabiashara Rais Samia ametoa milioni 100 ili lijengwe paa la kudumu kwa bati la kisasa.
Kutokana na fedha kupatikana, RC Makalla amewaelekeza Suma JKT ambao ndio wajenzi kuanza ujenzi mara moja ili Wafanyabiashara hao wafanye biashara bila kero

0 comments:
Post a Comment