Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Tuesday, July 20, 2021

ALIYEKUWA MKURUGENZI WA MIPANGO (TAKUKURU) KURUTHUM MANSOOR AACHIWA HURU.


 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia kwa dhamana aliyekuwa Mkurugenzi wa Mipango wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kuruthumu Mansoor (57) aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi, dhamana hii ni baada ya kufutiwa mashtaka ya utakatishaji fedha.

Mapema mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) aliwasilisha ombi la kubadilisha hati ya mashtaka baada ya kumfutia Mshtakiwa huyo mashtaka ya utakatishaji fedha na hivyo kupewa dhamana.

Akisomewa masharti ya dhamana Mshitakiwa ametakiwa kuwa na Wadhamini wawili wenye barua na vitambulisho vya Taifa au vitambulisho vinavyotambulika watakaosaini  bondi ya shilingi milioni 20.

Mansoor ametimiza masharti hayo na kuachiwa kwa dhamana baada ya kukaa mahabusu kwa zaidi ya miaka miwil

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates