Niliamua kulipiza kisasi cha kifo cha mume wangu kwa kuanzisha urafiki na mtu aliyemuua, nikafunga nae ndoa na hatimaye nikalipikiza kisasi."
•
Mwanamke huyo anasema alijaribu kwa miaka mitatu kulipiza kisasi kutokana na kifo cha mume wake, na alifanya mipango madhubuti kutekeleza hilo.
•
Kwa mujibu wa Polisi, alitumia miezi sita kujaribu kulipiza kisasi, lakini iliposhindikana, akaamua kuangalia njia nyingine (Plan B), ambayo ilikuwa ni kujiweka karibu zaidi na Gulistan Khan ili alipize kisasi.
•
Mwanamke huyo aliamua kumtongoza muuaji wa mume wake kwa meseji za mahaba na ukaribu ukaanza na baadae wakaoana, ingawa kwa kutumia njia ya kumrubuni kimapenzi.

0 comments:
Post a Comment