Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Tuesday, July 20, 2021

POLSI WAFANIKIWA KUMUUA JAMBAZI MMOJA DAR ES SALAAM.

 


Usiku huu katikati ya Mtaa wa Tunisia na Barabara ya Ali Hassan Mwinyi maeneo ya Leaders Kinondoni Dar es salaam Polisi wamefanikiwa kumuua Jambazi aliyepora simu akiwa na Pikipiki, kuanza kumimina risasi hewani kwa Bastola aliyokua nayo.

Kamamda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Ramadhan Kingai amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kuuwawa kwa jambazi huyo.

Kamanda ameiambia @ayotv_ kwamba Jambazi huyo ameuwawa na Polisi waliokuwa doria wakiwa na mavazi ya kiraia ambapo walisikia sauti ya Mwanamke aliyeporwa simu na Majambazi wawili waliokua kwenye pikipiki moja, kelele hizo ziliwashtua Polisi waliokua doria karibu na kuanza kuwakimbiza Majambazi hao na kumpiga risasi mmoja wao huku mwingine akifanikiwa kukimbia.

“Nikweli huyo akiwa na mwenzake wakiwa kwenye pikipiki nyeusi yenye namba MC 502 CUV walimpora mwanamke mmoja simu, mwanamke huyo alikuwa akitembea kwa miguu” 

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates