skip to main |
skip to sidebar
KWA MARA YA KWANZA HALSEY AMEPOST PICHA YA MTOTO WAKE.
Hitmaker wa ngoma ya "Sorry" Ashley Nicolette Frangipane anayefahamika kwa jina lake la kazi kama Halsey @iamhalsey amepost kwa mara ya kwanza picha ya mtoto wake aliyejifungua Julai 14 mwaka huu.Kwenye ukurasa wake wa Instagram, #Halsey amepost picha akiwa amemlaza kifuani mtoto wake waliompa jina la 'Ender Ridley Aydin', chini akisindikiza na ujumbe uliosomeka..."Ninashukuru sana kwa uzao huu nadra sana lakini wenye kuleta furaha" akimalizia na jina la mtoto wake na tarehe aliyozaliwa.Huyu ni mtoto wa kwanza kwa #Halsey na mpenzi wake Alev Aydin ambae ni muandishi wa filamu nchini Marekani, baada ya wawili hao kuwa na uhusiano tangu Oktoba mwaka jana.
0 comments:
Post a Comment