Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Tuesday, July 20, 2021

WASANII WALIOINGIZA HELA NYINGI KWA MWAKA 2020.


 Kuna usemi mmoja unasema, kama ikitokea maisha yakakupa malimao, basi yakamue utengeneze juice unywe upate Vitamin C, ndicho ambacho kimetokea kwenye list mpya ya wasanii wa muziki walioingiza mkwanja mrefu kwenye kazi zao, iliyotolewa na Billboard.


Licha ya kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa wa Corona, uliosimamisha shughuli zote zenye asili ya kukusanya watu pamoja, ikiwemo matamasha ya muziki, bado haikuzuia wasanii mbalimbali kutumia fursa ya kuwepo kwa mitandao ya kustream nyimbo zao kujiingizia pesa ya kutosha.

List ya wasanii 35 iliyotolewa na Billboard jana, imewashuhudia wasanii wakongwe kama Celine Dion na The Beatles wakirudi kwenye chart na tena kukaa nafasi za juu.

Kwa mujibu wa Billboard, mapato yaliyotokana na kufanya show yamepungua kutoka $779 Milioni kwa mwaka 2019 hadi $79 Milioni ikiwa imechangia 20% tu kwenye pesa walizoingiza wasanii kwa mwaka 2020.

Top 10 inakamilishwa na;

1. Taylor Swift $23.8m

2. Post Malone $23.2m

3. Celine Dion $17.5m

4. Eagles $16.3m

5. Billie Eilish $14.7m

6. Drake $14.2m

7. Queen $13.2m

8. The Beatles $12.9m

9. Young Boy Never Broke Again $11.9m

10. Lil Baby $11.7m

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates