Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Tuesday, July 13, 2021

NIGERIA; WATEKAJI WAMUACHIA HURU KIONGOZI WA KIISLAMU.


 Kiongozi maarufu wa kiislamu, Emir Alhassan Adamu, ambaye alitekwa Jumamosi na wanaume wenye silaha kaskazini magharibi mwa Nigeria katika jimbo la Kaduna, ameachiwa huru.

Ndugu zake kumi na mbili ambao walichukuliwa pia , wameachiwa pia.

Haijawekwa wazi namna Emir Adamu alivyopata uhuru wake lakini mtoto wake wa kiume ameiambia BBC kuwa watekaji hawakulipwa fedha.

Kumekuwa na matukio mengi ya utekaji kaskazini mwa Nigeria na kukiwa na wanafunzi zaidi ya 1,000 wakiwa wametekwa kutoka shuleni au vyuoni tangu mwezi Desemba.

Ingawa watu wengi wanaotekwa uachiwa huru mara baada ya watekaji kulipwa fedha, ingawa mpaka sasa tisa wamefariki na watu wapatao 200 hawajulikani walipo.

Utekaji nyara kwa ajili ya kupata fedha imekuwa biashara inayokuwa kwa kasi , na inasadikiwa kuwa wahuni hao huwa wanapata msaada kutoka kwa wanaijeria wenye wadhifa wakiwemo wakala wa usalama

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates