Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amemhakikishia Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango kuwa Wakulima wote wa zao la Korosho waliopewa ruzuku ya pembejeo kwa ajili ya kilimo cha msimu ujao hawatodaiwa wala kukatwa makato ili kugharamia pembejeo hizo kwani Serikali imezitoa bure kwa Wakulima lakini amewataka Wakulima kuendelea kuhudumia zao la korosho. Akizungumza katika mkutano Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara Naibu Waziri Bashe pia ameeleza kuwa ifikapo hadi mapema mwakani (2022) pembejeo zote kwa ajili ya msimu ujao wa kilimo zitakuwa zimeshafika katika maghala ya maeneo husika tayari kuwafikia Wakulima kwa wakati ili kuwaepusha na usumbufu.
Awali Makamu wa Rais, Dkt Philip Mpango ameitaka Wizara ya Kilimo kusimamia ubora wa Korosho na ameahidi kusaidia kuunganisha uongozi wa mikoa inayozalisha korosho pamoja na Balozi za Tanzania nje ya Nchi kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ili kuwezesha korosho ya Tanzania kuuzwa kwa wingi nje ya Nch

0 comments:
Post a Comment