Mbunge wa Kawe (CCM) na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima ameanza kampeni za kupinga chanjo ya Corona kutumika nchini Tanzania.Gwajima anadai Taifa lilikuwa na maono yake kuhusu chanjo na lilikataa chanjo toka mapema (kipindi cha Rais Magufuli) hivyo lingeendelea kukataa chanjo hizo.
Pia anadai chanjo zinazotolewa nchi za Ulaya ni tofauti na zilizokuja nchini, na hakuna Daktari wa kitanzania aliyefanyia utafiti chanjo hizo 'Chemical Content Analysis'.
Ameenda mbali na kusema kuna Watanzania wanatumika kuchanjwa chanjo bandia ili tu kuwaamasisha wengine wachanje chanjo halisi (anazodai ni mbaya).
Aidha, katika hali ya kushangaza amesema anaomba Mtu yeyote atakayechanja chanjo hizo na apoteze maisha.
Gwajima ameyasema hayo akiongea na Wahumini wa Kanisa lake kwa niaba ya Watanzania wote.

0 comments:
Post a Comment