Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Wednesday, July 14, 2021

N-SPORT; TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA.

 


 Barcelona wanakaribia kukamilisha mpango wa kumpeleka mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, 30, kwenye klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid ili iweze kumnasa kiungo wa kati wa Uhispania Saul Niguez, 26. (Mail)


Everton imewasilisha du la mwanzo kumsajili mchezaji wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly, 30 ambaye anaripotiwa kuwa miongoni mwa wachezaji wanaolengwa na maneja Rafa Benitez(Calciomercato)

Liverpool wanaripotiwa kutenga pauni milioni 60 kwa ajili ya kiungo wa kati wa Inter Milan Nicolo Barella, 24. (La Repubblica)

Chelsea inataka kumtoa mshambuliaji Tammy Abraham,23, kwenda Borussia Dortmund kama sehemu ya makubaliano ya kumchukua mshambuliaji wa miaka 20 Erling Braut Haaland. (Mirror)

West Ham wako mbioni kuridhia makubaliano ya mkopo,kwa kumnunua mlinda mlango wa Ufaransa wa Paris St-Germain Alphonse Areola, 28. (Evening Standard)

Mlinzi wa Arsenal Hector Bellerin bado hajakubaliana na Inter Milan lakini klabu hiyo ya Italia ina mpango wa kumnasa Mhispania huyo mwenye miaka 26. (Football.london)

kiungo wa kati wa Arsenal Joe Willock,21, ameripotiwa kuiambia klabu hiyo kuwa atajiunga tena na Newcastle kwa mkopo kwa ajili ya msimu mpya wa ligi ya Primia. (Daily Express)

Leicester City wametoa ofa kwa mchezaji wa Ubelgiji Youri Tielemans, 24, ya mkataba wa muda mrefu na wanaamini kiungo huyo wa kati atasalia katika klabu hiyo, ingawa Liverpool wanamuhitaji.(Telegraph)

Kocha wa Roma, Jose Mourinho anaweza kuigeukia Old Trafford kuongezea nguvu kikosi chake msimu huu wa joto, huku kocha huyo wa zamani wa United akimtolea macho beki wa kushoto wa Brazil Alex Telles, 28, kama mbadala wa Leonardo Spinazzola aliye majeruhi. (Daily Star)

Arsenal inajiandaa kumkosa mshambuliaji wa PSV Eindhoven Mholanzi Donyell Malen, 22, baada ya kufikia makubaliano ya kujiunga na Borussia Dortmund kama mbadala wa Jadon Sancho (Just Arsenal via Sports Bild).

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates