Kocha Mkuu wa @simbaqueensctz Mussa Hassan Mgosi kupita ukurasa wake wa Instagram amethibitisha kupokea zawadi ya gari kutoka kwenye uongozi wa Simba sports club na amewashuruku kwa zawadi hiyo.
Hiki hapa alichokiandika @officiall_mussamgosi kwenye ukurasa wake wa Instagram
"Asante Simba Sports Club kwa zawadi ya Gari ila makabidhiano naomba yawe siku ile ya mechi ya SIMBA S.c wakikabidhiwa kombe la V.P.L hii itasaidia kwa wachezajikuiga maadili ya kuitumikia Simba kwa nidham na uadilifu
Pia nichukue fursa hii kuwashukuru TFF na Benchi la TWIGA STARS na UONGOZI wa SIMBA kwa kufanikisha mechi ya jana kwa jili Simba Queens KUPATA MECHI ya kujipima na kuiangalia nini kifanyike kabla ya mchuano ya kimataifa kuanza matokeo ni kitu kingine ila naamini kwa ukanda wa CECAFA NGAZI ya vilabu akuna team bora yenye cream ya wachezaji bora kama team ya Taifa ambayo tumecheza jana hivyo niendelee kuomba tupate kucheza mechi hiyo kwa mara nyingine zaidi kutakapo kuwa na nafasi ya hilo lengo ni kuijenga Simba Queens kwakuwa wana jukumu la kitaifa na team TAIFA TWIGA STARS wanajukumu la TAIFA"

0 comments:
Post a Comment