Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Thursday, July 15, 2021

N-SPORT; MESSI AFANYA MAAMUZI YA KUBAKI BARCELONA HADI MWAKA 2026.


Mshambuliaji wa Argentina, Lionel Messi amekubali kusalia Barcelona kwa kandarasi ya miaka mitano ambayo itamfanya kusalia hapo hadi mwaka 2026.


Kwenye makubaliano hayo mapya yanahusisha pamoja na kupunguza nusu ya mshahara wake kwa asilimia 50.

Tangazo hilo linategemea kuondoka kwa wachezaji ambapo litaiwezesha Barca kufadhili mshahara wa nahodha huyo wa Argentina.

Mshindi huyo mara sita wa tuzo za Ballon d'Or amekuwa mchezaji huru tangu kumaliza kwa mkataba wake ndani ya Barcelona mwezi June 30 wakati alipokuwa akilipwa paundi milioni 123 kwa msimu.

Hata hivyo Messi kwa sasa yupo mapumzikoni baada ya kushinda taji la Copa America na maelezo ya ndani kuhusu kandarasi hiyo hayajakamilishwa.

Kumshawishi Messi kusalia katika klabu hiyo ndio lililokuwa lengo la mwenyekiti mpya wa klabu hiyo Joan Laporta.

Barca pia inatazamia makubaliano ya kubadilishana wachezaji yanayohusisha uhamisho wa mshambuliaji Antoine Griezmann na kiungo wa kati wa Atletico Madrid Saul Niguez , ili kupunguza matumizi ya mishahara ya wachezaji.

Wchezaji kama vile Junior Firpo, Jean Clair Todipo na Carles Alena tayari wameuzwa ili kupunguza matumizi lakini pia uuzaji wa wachezaji wenye majina makubwa pia utafanyika.

Messi alihusishwa na uhamisho wa kuelekea PSG na Manchester City , ambapo angekutana tena na mkufunzi wa zamani wa Barcelona Pep Guardiola , pamoja na ligi ya MLS nchini Marekani ambapo alisema kwamba huenda akaichezea katika siku za usoni.

Messi ndiye mfungaji bora kuwahi kuonekana Barcelona akiwa na magoli 672 na kushinda mataji 10 ya La Liga, mataji manne ya klabu bingwa Ulaya mataji saba ya Copa del rey pamoja na kuwania taji la Ballon d'Or kwa mara ya sita.

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates