Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Friday, July 23, 2021

MISONGAMANO MARUFUKU TAARIFA YA WAZIRI WA AFYA MHE, DOROTHY GWAJIMA.

 


 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Dorothy Gwajima amesema kuanzia jana July 22,2021 amepiga marufuku shughuli zote za misongamano yote isiyo ya lazima na ile yenye ulazima tahadhari ya kutosha ichukuliwe bila kuathiri shughuli za kiuchumi na Kitaifa.


Katika taarifa yake amesema “Nimekataza shughuli zote za misongamano yote isiyo yenye ulazima kuanzia July 22 2021 na ile ya ulazima tahadhari ya kutosha ichukuliwe bila kuathiri shughuli za kiuchumi na kitaifa”

“Naelekeza Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuwapa ushirikiano Waganga Wakuu wa mikoa na Wilaya kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria ya Afya ya Jamii na kuweka utaratibu mzuri kwa wale wanaoomba vibali vya shughuli zenye ulazima” ——— Dr. Doroth Gwajima, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates