Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Friday, July 23, 2021

DK. ABBAS WA COSOTA AAGIZA MSANII MB DOGG APATIWE HAKI ZAKE.

 


Katibu mkuu wa Wizara ya Habari Dkt. Hassan Abbasi ameiagiza Taasisi ya Hakimiliki Nchini (COSOTA) kufuatilia na kuhakikisha msanii Mb Dogg @mbdogg_master anapata haki zake kutoka kampuni ambazo zimetumia kazi zake bila yeye kupata chochote.


Dkt. Abbasi ametoa maagizo hayo alipomwita msanii huyo aliyekuwa amelalamika kwenye ukurasa wake wa Instagram akiomba msaada wa kupiganiwa haki zake.

“Hili limeisha COSOTA simamieni msanii huyu apate haki zake kutoka kampuni za ZIIKI na kampuni nyingine iitwayo ZEZE ambayo iko Kenya hivyo mtawasiliana mara moja na wenzetu wa Kenya kuhakikisha kazi za Mb Dogg zinapata stahiki yake,” alisema Dkt. Abbasi.

Itakumbukwa, hivi karibuni @mbdogg_master kupitia ukurasa wake wa Instagram alieleza kuwa ameshangazwa na nyimbo zake nyingi zinatumika katika mitandao ya kuuza muziki bila aidha makubaliano au pale penye makubaliano bila kupewa stahiki zake.

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates