Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Friday, July 23, 2021

MOTO WATEKETEZA MJENGO WA KIFAHARI WA JAY_Z NA BEYONCE.

 


Mjengo wa kifahari wa familia ya mastaa Jay-z na Beyonce ulioko New Orleans Marekani umeripotiwa kushika moto usiku wa Jumatano ya tarehe 21.


Mtandao wa TMZ unaeleza kuwa, iliwachukua askari 22 wa zimamoto muda wa saa mbili kuuzima moto huo ambao chanzo chake bado hakijawekwa wazi.

Hakuna mtu yoyote ambae amedhurika kutokana na moto huo, na haijafahamika pia hasara rasmi iliyotokea baada ya kuungua kwa mjengo huo.

The Carters walinunua mjengo huo wa kihistoria wenye zaidi ya miaka 90 mwaka 2015 kwa gharama ya $2.6 Million, ambapo mwanzo lilikuwa ni jengo la kanisa na baadae kubadilika matumizi kuwa ukumbi wa kujifunza kucheza muziki kwa style ya ballet.

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates