Simba ambao walitwaa ubingwa huo Julai 11 baada ya kufikisha Alama 79 kufuatia ushindi wa mabao 2-0 walioupata dhidi ya Coastal Union FC itakabidhiwa Kombe hilo na Medali baada ya kumalizika kwa mchezo wao wa mwisho wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Namungo FC
Bodi ya Ligi imeipongeza klabu ya Simba kwa kutwaa ubingwa huo, Pia imezipongeza klabu zote shiriki kwa kuendelea kuonesha ushindani wa hali ya juu uliosaidia kuongeza ubora wa michuano hiyo ya mpira wa miguu inayoshika nafasi ya nane (8) kwa ubora barani Afrika

0 comments:
Post a Comment