Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Tuesday, July 13, 2021

BURUDANI; WIZKID NA TEMS WAWEKA REKODI BILLBOARD HOT100.

 


Wimbo wa @wizkidayo "Essence" ft. @temsbaby umeingia katika chart kubwa duniani za Billboard Hot 100

Ngoma hiyo imefanikiwa kuingia katika chart hizo na kukamata nafasi ya 82 ikiwa ni baada tu ya mkwaju huo kuuza nakala 40,000 nchini Marekani wiki iliyopitwa

Hii inakuwa mara ya tatu kwa mkali huyo wa Nigeria kuingia kwenye chart hizo, kwani kwa mara ya kwanza aliingia hadi namba 1 kupitia "One Dance" wimbo ambao alipewa shavu na Drake mwaka 2016, wimbo huo ulikaa namba 1 kwa wiki 10. Mara ya pili aliingia kupitia wimbo wa "Brown Skin Girl" alioshirikishwa na Beyonce.

Pia hii inakuwa ndio ngoma ya kwanza ya kutoka Nigeria kuingia katika Chart hizo kubwa duniani ambayo inamilikiwa na star huyo.

Vile vile #Tems anakuwa mara yake ya kwanza kuingia kwenye charts hizo za #BillboardHot100

Unadhani ni Star gani hapa nchini ataingia kwenye Chart hizo kubwa duniani ?

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates