Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Tuesday, July 13, 2021

HAITI; WAFANIKIWA KUMKAMATA ALIYE SABABISHA MAUAJI YA RAIS JOVENEL MOISE.







Polisi wa Haiti wametangazakuwa wamemkamata raia wa Haiti "ambaye alikuwa na malengo ya kisiasa" katika kuajiri watu wenye silaha waliomuua Rais Jovenel Moise wiki iliyopita.
"Huyu ni mtu ambaye aliingia Haiti kwa ndege ya kibinafsi kwa malengo ya kisiasa," Leon Leon, mkuu wa Polisi ya Kitaifa ya Haiti amesema.
Christian Emmanuel Sanon, mwenye umri wa miaka 63, ambaye ni raia wa Haiti, aliwasili katika kisiwa hicho mnamo Juni akiandamana na Wakolombia kadhaa, kulingana na maelezo yaliyotolewa kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Mawaziri kadhaa wa Haiti pia walikuwa kwenye mkutano huo.
"Ujumbe huo ulibadilika," Charles alisema, akielezea kuwa nia hapo awali ilikuwa kukamata Moise, na operesheni hiyo iliongezeka kutoka ndani ya nchi.
"Watu wengine ishirini na wawili waliingia Haiti," Charles alisema.
Raia kumi na nane wa Colombia wamekamatwa tangu Jumatano. Kwa kuwahoji, polisi wa Haiti waligundua kuwa Sanon alikuwa ameajiri washiriki wa timu 26 kupitia kampuni ya usalama ya Venezuela inayoitwa CTU.
Hakuna maafisa wa polisi waliojeruhiwa wakati wa shughuli za kuwakamata watu wanaodaiwa kuwa mamluki wa Colombia, watatu kati yao waliuawa katika mchakato huo.

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates