Huenda mashabiki wa klabu ya PSG wakawa wamezima uwezekano wa Supastaa wa Manchester United, Paul Pogba kujiunga na klabu hiyo ambayo amekuwa akihusishwa nayo tangu aliporipotiwa kugomea mkataba mpya Old Trafford.Hii ni baada ya Jumamosi iliyopita, mashabiki wa PSG kuweka bango nje ya uwanja wa klabu hiyo pamoja na ule wa mazoezi wakipinga Paul Pogba kujiunga na timu yao kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.
Bango lililowekwa nje ya Uwanja wa Parc des Princes lilisomeka: “Pogba msikilize mama yako, hataki uje hapa. Hata sisi hatutaki pia!”
Kwa taarifa za ndani ambazo zimewekwa wazi kupitia mtandao wa Daily Mail zinasema kuwa Mama mzazi wa Pogba hataki kusikia kabisa tetesi za Pogba kujiunga na PSG ni bora aende timu nyingine ila sio PSG kwani Pogba atachezea klabu ambayo ni Adui wa Marseille. Kwa kuwa wazazi wake walikuwa mashabiki wa Marseille

0 comments:
Post a Comment