Kalamu ya @swalehmawele
Pascal Wawa huwa anaipa Simba chaguo la pili katika kushambulia na ni mchezaji muhimu katika safu ya ulinzi ya Simba nyuma ya Joash Onyango.
Falsafa ya Simba ni kupiga pasi fupifupi kuelekea mbele lakini si kweli kwamba watacheza katika aina hii ya mpira kwa dakika zote 90, kuna muda wanatakiwa kubadilika na hapa ndipo anapokuja Pascal Wawa.
Katika hali ya kawaida unapokuwa katika mstari wa kwanza wa kuanzisha mashambulizi unakuwa na nafasi kubwa ya kuiona timu nzima na ilivyojipanga na kujua ni pasi ipi ya kwanza itakuwa na madhara endapo utaipiga.
Ni hapa ambapo hata walinda milango wanashauriwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuanzisha mashambulizi, mbele ya Pep Guardiola Ederson ni kipa bora kuliko David Degea kutokana na system yake.
Pascal Wawa anacheza chini na mara nyingi amekuwa akipiga pasi zinazoharakisha mashambulizi kwa kuua karibu mistari miwili au mitatu ya ulinzi na mpira kufika haraka katika eneo la hatari la wapinzani.

0 comments:
Post a Comment