Tuesday, July 20, 2021
MAJARIBIO YA TRENI YA UMEME YATAANZA NOVEMBER MWAKA HUU 2021.
“Hayati JPM aliacha miradi ambayo Rais Samia alisema lazima imalizike na mingine ianze, mfano Hayati JPM alianza mradi wa kujenga reli Dar hadi Morogoro na ilifika 86% ila sasa mradi umefika zaidi ya 92% na mwezi November treni ya umeme itafanyiwa majaribio"
“Ujenzi wa SGR umefikia 92% na mwezi November,2021 treni ya majaribio itatoka Dar es Salaam kwenda Morogoro na kutoka Morogoro kwenda Singida ambako ujenzi wake umefikia 65 %”
“Reli kutoka Mwanza - Isaka fedha ya awali TZS Bilioni 372 imeshatolewa na kazi inaendelea, Rais Samia amewaagiza TRC kuanza maandalizi ya kutafuta Wakandarasi wa kuanza kujenga kutoka Makutupora - Tabora - Isaka - Kigoma - Kaliua - Mpanda- Kalema”———Msemaji Mkuu wa Serikali, @gersonmsigwa kwenye Clouds360 ya @cloudstv
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment