Thursday, July 15, 2021
JUMA NATURE ATANGAZWA KUWA BALOZI WA WILAYA YA TEMEKE .
Meya wa Manispaa ya Temeke Abdallah Mtinika leo Jumatano (Julai 14) amemtangaza Msanii mkongwe wa Bongo fleva Juma Nature (@sir_nature) kuwa Balozi wa Wilaya ya TEMEKE iliyopo Jijini Dar Es Salaam. Nature ambaye aliwahi kutoa maoni hasi juu ya mchekeshaji wa Kenya Eric Omondi kupewa Ubalozi wa Wilaya hiyo, kupitia instagram ameandika:-
"Asante Mh meya @abdallah_mtinika kwa kunitambua na kunithamini kuniteua kuwa balozi wa TEMEKE Leo hii." --- ameandika @sir_nature. Aidha kwa upande wa Meya Abdallah Mtinika, ameandika
-
"Leo ni siku kubwa sana kutembelewa na Legend wa TMK ,sir nature hakika tumezungumza mengi sana juu ya kupambania Temeke yetu ktk mambo mengi, Leo Nimekutangaza rasmi kuwa balozi wa Temeke kikwazo kilikuwa muda tu wa kuja rasmi kukupa bendera yako lkn tayari wewe ni balozi wa Temeke tangu tulipoanza kutumia maandishi matatu (TMK) ,natumai utatusaidia kubeba ajenda za Temeke kama USAFI , WATU WARUDI SOKONI ,ULINZI NA USALAMA ,TEMEKE BILA MADAWA NA TEMEKE NA MAENDELEO PAMBANA MWANANGU TUPO TUNAANGALIA JUHUDI ZAKO ZA KIUBEBA TMK @sir_nature"
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment