Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Tuesday, July 20, 2021

DAVID BECKHAM ALIVYOSTAWISHA PENZI LAKE NA VICTORIA BECKHAM NA KUZIMA PENZI LA MIGUU YAKE KWA MPIRA!

 .


Fergie alipomuita ofisini alimuambia Beckham maneno machache mno na sanasana alimshauri aachane na Victoria Posh. Hakupenda uhusiano wao ambao ulitawaliwa na matangazo mengi kwenye vyombo vya habari. Aliamini Becks anajitoa kwenye reli. Lakini Becks alikataa katakata kuhusiana na hilo.

.
Inasemekana babu wakati huo alikaa na Riwaya ya “Ngoswe Mapenzi kitovu cha uzembe” (natania 😂) akiamini kabisa Victoria hakua mwanamke sahihi Kama Beckham atataka kucheza mpira kwa muda mrefu.
.
Msimu wa 2002-03 kupungua kwa uwezo wa Beckham kukaanza kuonekana na hiyo ilichagizwa na United kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Arsenal ambapo kiwango cha Beckham kilikua cha chini mno.
.
Sasa wakati wameenda katika vyumba vya kubadili nguo Becks akiwa amekaa, Fergie alimuambia kuhusu kiwango chake kwa ukali sana na kwakua chini kulikua na viatu vingi babu alikipiga kimojawapo na kikamkuta Beckham usoni.
.
Na huo ndio ukawa mwanzo wa mwisho wa maisha murua ya Beckham na United. Fergie aliandika “Ule mda ambao mchezaji atahisi yeye ni mkubwa kuliko United ndio ndio mda anaotakiwa kuondoka...Beckham alichagua maisha ya ustaa nje ya uwanja kuliko kipaji chake. Na sikuona pengo yeye akiondoka”
.
Beckham alishawahi kukiri hilo kwani baada ya kuuzwa Madrid na Baadae AC Milan ambalo alipewa uhuru wa maisha hakucheza mpira kwa muda mrefu. Akatimkia ligi ya Marekani.
.
Ikumbukwe msimu huohuo wa mwaka 2003 ndio Fergie alimsajili Kinda Cristiano Ronaldo ambae ni kipenzi chake kutoka moyoni kwa jinsi ambavyo alifuata maelekezo yake.!
.
Na huo ndio ukawa mwanzo wa mwisho wa English Prince David Beckham 👊⚽️

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates