Social Icons

NIFA AD

NIFA AD

NIFAAAA

NIFAAAA

Tuesday, July 20, 2021

ROONEY & RONALDO NA KISA CHA MAISHA YAO!


 Siku za mwanzo za maisha yake ya soka katika EPL zilikua ngumu sana kwa Ronaldo kutokana na matumizi makubwa ya mabavu katika ligi hiyo. Wayne Rooney alikaririwa akisema “Nilikua kila siku nampitisha Ronaldo katika maduka ya Mac Donald’s ili aweze kula Big Mac aongeze uzito wa mwili wake, kwani alikua mwepesi mno” Walikua maswahiba wa kufa na kuzikana!

.
Wakiwa makinda wa timu mwaka 2006 katika kombe la Dunia lilitokea tukio lililogonga vichwa vya habari ambapo, Wayne Rooney alimchezea rafu Ricardo Carlvalho katika mchezo wa robo fainali Kati ya England na Ureno. Cristiano alilalamika sana kwa mwamuzi Horacio Elizondo huku akisisitiza Rooney apewe kadi nyekundu
.
Wayne alipewa kadi nyekundu na England ilitolewa kwa mikwaju ya penati. Rooney Anasema akiwa amekaa na simu yake alipokea meseji nyingi kumhusu Ronaldo. Na wakimshinikiza chuki za waziwazi kwake!
.
Baada ya mechi kwisha Ronaldo na Rooney walikutana papo hapo na waliongea maneno machache sana. Rooney hakutegemea yale kutoka kwa rafiki yake wa kupika na kupakua kiasi cha kubadilishana namba za mashati wawapo mazoezini. Mara nyingi wakati wa mazoez Rooney alivaa shati namba saba huku Ronaldo akivaa namba kumi
.
Unataka kujua waliambizana nini? Ronaldo alibakia na tatizo kubwa nchini uingereza. Unataka kujua ni tatizo lipi? Na nini kilimtokea? Je Maneno yasiyopungua kumi kutoka kwa Rooney kwenda kwa Ronaldo Alimueleza nini?

0 comments:

Post a Comment

 
 
Blogger Templates